Showing posts with label Gene Siskel Film Center. Show all posts
Showing posts with label Gene Siskel Film Center. Show all posts

Wednesday, August 13, 2008

Bongoland II itaonyeshwa Chicago Ijumaa


Kibira Films inawatangazia kwa mara nyingine kuwa BONGOLAND II inaonyeshwa ijumaa hii mjini Chicago. Unakumbushwa kuja kuiona sinema ambayo kwa kweli imeonyesha ukomaaji wa fani ya usanii wa sinema katika Tanzania.
Watu wengi waliooiona sinema hii wameipenda sana. ANGALIA MAONI HAPABONGOLAND II itaonyeshwa saa kumi na mbili na robo Ijumaa hii tarehe 15.Ukumbi ambapo sinema hii itaonyeshewa ni GENE SISKEL FILM CENTER. Mkurugenzi wa sinema hii atakuwapo katika ukumbi kujibu maswali mwishoni.Anwani ya Ukumbi ni 164 North State Street Chicago Il 60601
SIMU YAO NI - 312-846-2600 KARIBUNI!!

Tuesday, July 15, 2008

Josiah Kibira alinganishwa na Sembene Ousmane!

Wadau, Mtengeneza sinema wa kiTanzania, Josiah Kibira amelinganishwa na mtengeneza sinema maarufu wa kiafrika, marehemu Sembene Ousmane. Gene Siskel Film Center ambayo inatambulika hapa Marekani kama sehemu maarufu inayotoa maoni juu ya sinema inasema kuwa sinema, Bongoland II ni kama aina ya sinema ambazo alitengeneza marehemu Sembene. Inafanya mtazamaji afikirie kwa undani.

Kati ya watengeneza sinema wote wa kiafrika, Sembene ndiye anajulikana zaidi kwa ajili ya sinema zake kama Moolaade, Xala na Faat Kine.

Bongoland II itaonyeshwa Chicago mwezi ujao, na Detroit hivi karibuni, tarehe za Detroit bado hatujapata.

**********************************************************************


BONGOLAND II: THERE’S NO PLACE LIKE HOME 2008,
Josiah Kibira, Tanzania, 100 min.
With Peter Omari, Thecla Mjatta

In his first film BONGOLAND (2003), Josiah Kibira related the misadventures of Juma, a Tanzanian immigrant in Minnesota. In this self-sufficient sequel, Juma returns to Tanzania (aka Bongoland) to manage a company. His American-style ideas about efficiency and motivation meet with a less than enthusiastic response, and, when Mom’s visit produces some jaw-dropping revelations, he discovers that his relationship to his homeland has become even more tenuous. The film’s sharp, angry satire recalls such Ousmane Sembene classics as XALA and GUELWAAR. In Swahili with English subtitles. DV-CAM video. (MR)

Itaonyeshwa mjini Chicago:

164 North State Street
Chicago, Illinois 60601

Tel: 312-846-2600

MOVIE HOTLINE: 312-846-2800

Itaonyeshwa mara mbili:

Ijumaa/Friday, August 15, 6:15 pm
Jumatano/Wednesday, August 20, 6:15 pm