
Khawad ndo aliwaambia polisi kuhusu darasa la Mwalimu Gibbons kuita mdoli, Mohamed na kusababisha matatizo yote. Unity High School imefungwa kwa muda.
Blogs in Kiswahili, the main African language of EAST AFRICA.
Macho ya waiingereza yamekuwa Sudan tangu jumapili kwa sababu ya mwalimu kutoka Uiingereza anayefundisha katika shule ya International huko. Mwalimu Gillian Gibbons ana miaka 54. Wanafunzi wake wana miaka saba na lazima bado wako kwenye umri wa kupenda toys (vitu vya kuchezea). Walikuwa na mdoli wa darasa. Aliwapa zoezi la darasa kumpa jina. Wengi walichagua jina Mohamed. Kwa kidemokrasia wengi wanashinda. Hao watoto wa miaka 7 ndo waliochagua jina la Mohamed. Majina mengine yaliyopendekezwa ni Hassan na Abdullah.
Huyo mwalimu namhurumiwa sana. Lazima hakuelewa uiislamu vizuri. Hakuna picha ya mtume Mohamed na wala hakuna sanamu yake. Hivyo kumwita huyo mdoli Mohamed ilikuwa tusi kubwa kwa waislamu. Pia kaanza kufundisha Sudani juzi juzi tu. Kwa wazungu kutoa jina kwa midoli ni kawaida. Sasa anashitakiwa kwa kosa la kutukana uislamu.
Sasa nauliza hivi, hao waSudani hawakuweza kumwelezea kuwa kafanya kosa na kumwelimisha. Baadala yake walitishia kumchapa viboko 40 na kufungwa jela.
Leo mahakama huko wameamuru afungwe siku 15 na awe deported akitoka. Tayari waSudani wanaonekana wabaya duniani kwa kuua raia wao wanye asili ya Afrika hasa kabila la Dinka huko Darfur.
Nawauliza wasomaji waislamu, je, walivyofanya waSudani ni sawa au walizidisha kipimo na hii tukio?
Na hao watoto je, waadhibiwe kwa kuchagua hiyo jina au waelimishwe sheria za uisilamu? Lazima wataathirika maishani mwao wakikumbuka mwalimu wao mpendwa alivyonyanyaswa kwa kosa hiyo.
Hii kesi inasisitiza umuhimu wa watu wanaoenda nchi zingine kuelewa mila na desturi na dini za huko!
Kwa habari zaidi someni:
http://www.cnn.com/2007/WORLD/africa/11/29/sudan.bears/index.html
http://www.abcnews.go.com/International/story?id=3931681&page=1
http://www.cfnews13.com/News/International/2007/11/29/briton_convicted_in_sudan_blasphemy_case.html