Showing posts with label Hongera Mwanangu. Show all posts
Showing posts with label Hongera Mwanangu. Show all posts

Monday, July 22, 2013

Mama Bishanga Ampongeza Natasha!



Mimi mama Bishanga na mwanangu Kilian Kamota tunakupa hongera kwa kazi nzuri uliotimiza
ya kufunga ndoa nasi huku tulikuwa tunasherekea ndoa pia ya wa tz wenzetu siku hiyo.

Uliniahidi mwaka 2011nilipokuja TZ kufunga ndoa kuwa nawe utafanya hivyo. Umetimiza ahadi
ya Mungu ya kuungana mume na mke kuwa kitu kimoja halali. Mmependeza sana mdogo wangu
tunza mzee wako, mapenzi ya uzeeni matamu sana. Mpe raha mumeo.

Christina Innocent / Mama Bishanga

OHIO

USA

Thursday, September 24, 2009

Maneno ya Wimbo 'Hongera Mwanangu'

Bibi Titi na Mwalimu Nyerere

Kuna mdau kaniomba nimtafutie maneno (lyrics) za wimbo, Hongera Mwanangu ambayo tulisikia sana Radio Tanzania enzi zile ukiimbwa na marehemu Bibi Titi Mohamed. Sasa naomba nisaidie, ni lugha gani wanaiyotumia. Naona maneno ya kiswahili na sijui ni kilugha gani.


******************************************************************

HONGERA MWANANGU

Hongera mwanangu eh hongera.
Nami nihongeree hongera.

Hongera mwanangu eh hongera.
Nami nihongeree hongera.

Mama uchungu, Mama uchungu.

Nyamara mwanangu. Oyee.

Nyamara mwanangu tumbo la udere linauma mno eh!