Showing posts with label Jerry Isaac Mruma. Show all posts
Showing posts with label Jerry Isaac Mruma. Show all posts

Monday, December 30, 2013

Shukurani Kutoka Familia ya Isaac Mruma

Familia ya Mruma ya Dar es Salaam na Ugweno, Mwanga inatoa shukurani nyingi
kwa ndugu,jamaa,marafiki, majirani na Watanzania wote waliojitokeza kuwa
nao kwa njia tofauti katika kipindi cha msiba wa mtoto wao mpendwa Jerry
ambaye alifariki dunia Nairobi tarehe 17 Novemba na kuzikwa Dar es Salaam
tarehe 26 Novemba 2013.



Ni vigumu kutoa shukurani hizi kwa majina. Kwa njia ya kipekee, tunaomba
tuwataje wachache kwa niaba ya wote kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Balozi wa Tanzania Kenya Mh. Dr. Batilda Burian na wafanyakazi
wa ubalozi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya magazeti ya Serikali ( Daily News na
Habari Leo); Uongozi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha USIU, Nairobi; Lee
Funeral Home, Nairobi; Bwana na Bibi Mutinda wa Athi River, Nairobi; Bwana
na Bibi Ouma wa Kitengela, Nairobi; Hoteli ya Ololoitikoshi
Resort, Kitengela; Mchungaji Kiongozi na wazee wa Usharika wa Mbezi Beach
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jumuiya ya Betheli,
Mbezi Beach; Mheshimiwa CD Msuya; Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika
Mashariki - Mh. Angela Kizigha, Mh. Nderakindo Kessy, Mh.Shyrose Bhanji,
Bwana na Bibi Kachenje wa Mbezi Beach; Swissport Dar es Salaam; Qnet
Kenya; Love Titans - Nairobi, Kenya; Kibosho Girls Reunion, Mbezi Beach Family.

 
Katika kipindi kama hiki ni rahisi kuishiwa na maneno ya kuelezea faraja
tuliyopata kwa namna mlivyokuwa nasi wakati wote na pia mlivyotuombea.
Maneno pekee yanayokuja haraka ni AHSANTENI SANA, MUNGU AENDELEE
KUWABARIKI.









Friday, November 22, 2013

Tanzia - Jerry Isaac Mruma (1990-2013)

The Late Jerry Isaac Mruma

Ninakushukuruni marafiki zangu, ninazishukuru blogu na tovuti zote zilizotoa tangazo la kumtafuta Jerry Isaac Mruma, na yeyote kwa namna yoyote aliyotoa ushirikiano kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kusali, kuomba na kutoa maneno ya kutia faraja katika kipindi chote tokea Jumapili hadi kufikia leo, Ijumaa, Novemba 22, 2013 ambapo mwili wa Jerry umepatikana.

Habari zaidi zitatolewa na familia itakapokuwa tayari.

Asanteni.

Subi|wavuti.com
********************************************************
Wadau, nilifanya kazi Daily News na baba yake Jerry, Mzee Isaac Mruma.  Nakumbuka Isaac alivyooa na Jerry kuzaliwa. Jerry amefariki Kenya alipokuwa anasoma MBA.  Nimesikia kuwa Jerry ameuawa kwa kunyongwa karibu na Chuo aliyokuwa anasoma. Nangojea taarifa zaidi.
 
Poleni sana Mzee Isaac Mruma na familia.
REST IN ETERNAL PEACE JERRY MRUMA

- Chemi Che-Mponda

Thursday, November 21, 2013

Help Find Jerry Mruma - Missing in Kenya


Jerry Isaac Mruma (Age 23)

Jerry Isaac Mruma is a Tanzanian USIU-Africa Student (in Kenya) who went missing on Saturday night. (You may click here to watch him in this video)

Jerry had left the Tanzania Night at Pan Afrique Hotel and spoke to his friend Ogwellah at around 11:40PM

Another friend tells that Jerry had called her to inform her that he was on his way home. Unfortunately, he never got there. She has not heard nor seen Jerry since Saturday and calls to his phone aren't going through. She has filed a report with the Police for missing persons.

If you see or hear from Jerry anywhere please let us know.

Kindly call 0710 691 252 or click here to report to USIU Students Affairs Office.


Help us find JERRY ISAAC MRUMA.