Showing posts with label John Atchinson. Show all posts
Showing posts with label John Atchinson. Show all posts

Saturday, October 06, 2007

Baba mwenye miaka 53 ataka kufanya ngono na mtoto wa miaka mitano!

Mwendesha Mashtaka (Prosecutor) wa Serikali John David Roy Atchinson

Huyo baba pichani juu, John David Roy Atchinson, mwenye miaka 53, alijiua jana akiwa amefungwa jela huko Detroit, Michigan.

Atchinson alikuwa anafanya nini Michigan wakati kwao ni Golf Breeze, Florida? Mwezi iliyopita alipanda kwenye ndege kwenda Detroit kwa nia ya kufanya ngono na mtoto wa kike mwenye miaka mitano. Alikuwa ana 'chat' kwenye internet na mtu aliyedhania ni mama wa huyo mtoto. Huyo mama alidai kuwa anauza binti yake kufanya ngono na watu. Kumbe huyo mama feki alikuwa ni polisi!

Sasa polisi wanasema kuwa Atchinson alitua kwenye uwanja wa ndege (Metropolitan Airport) huko Detroit akiwa na zawadi ya dolly aina ya Dora the Explorer, hereni kubwa na mafuta aina ya vaseline! Alikamatwa hapo hapo uwanja wa ndege.

Alivyofika mahakamani alikana mashitaka dhidi yake. Ajabu Atchinson mwenyewe ni mwendesha mashtaka wa serikali huko Florida.

Atchinson ameacha mke ambaye ni mwalimu wa shule na watoto wa tatu. Watu huko florida wanasema kuwa hawakuhisi hata kidogo kuwa kuyo Atchinson yuko hivyo. Alikuwa kocha wa timu za michezo za watoto wake. Pia alikuwa ni rais wa chama cha michezo huko Florida.

Kwa habari zaidi za hiyo tukio soma:

http://www.usatoday.com/news/nation/2007-10-05-prosecutor-suicide_N.htm

http://www.nytimes.com/2007/10/06/us/06suicide.html

http://www.northcountrygazette.org/news/2007/10/05/pedophile_suicide/