Saturday, October 06, 2007

Baba mwenye miaka 53 ataka kufanya ngono na mtoto wa miaka mitano!

Mwendesha Mashtaka (Prosecutor) wa Serikali John David Roy Atchinson

Huyo baba pichani juu, John David Roy Atchinson, mwenye miaka 53, alijiua jana akiwa amefungwa jela huko Detroit, Michigan.

Atchinson alikuwa anafanya nini Michigan wakati kwao ni Golf Breeze, Florida? Mwezi iliyopita alipanda kwenye ndege kwenda Detroit kwa nia ya kufanya ngono na mtoto wa kike mwenye miaka mitano. Alikuwa ana 'chat' kwenye internet na mtu aliyedhania ni mama wa huyo mtoto. Huyo mama alidai kuwa anauza binti yake kufanya ngono na watu. Kumbe huyo mama feki alikuwa ni polisi!

Sasa polisi wanasema kuwa Atchinson alitua kwenye uwanja wa ndege (Metropolitan Airport) huko Detroit akiwa na zawadi ya dolly aina ya Dora the Explorer, hereni kubwa na mafuta aina ya vaseline! Alikamatwa hapo hapo uwanja wa ndege.

Alivyofika mahakamani alikana mashitaka dhidi yake. Ajabu Atchinson mwenyewe ni mwendesha mashtaka wa serikali huko Florida.

Atchinson ameacha mke ambaye ni mwalimu wa shule na watoto wa tatu. Watu huko florida wanasema kuwa hawakuhisi hata kidogo kuwa kuyo Atchinson yuko hivyo. Alikuwa kocha wa timu za michezo za watoto wake. Pia alikuwa ni rais wa chama cha michezo huko Florida.

Kwa habari zaidi za hiyo tukio soma:

http://www.usatoday.com/news/nation/2007-10-05-prosecutor-suicide_N.htm

http://www.nytimes.com/2007/10/06/us/06suicide.html

http://www.northcountrygazette.org/news/2007/10/05/pedophile_suicide/

1 comment:

Simon Kitururu said...

Kunawatu wagonjwa kwelikweli! Nashindwa kuelewa kabisa mtu anayemtamani mtoto kimapenzi.

Halafu inasemekana watu wengi wa aina hii hutamani watoto wadogo wa kiume, ndio kisa cha skendo la mapadre wa kiroma kuonyesha wengi wawalio waharibia maisha walikuwa watoto wa kiume.
Lakini ,ndio hivyo tena!Wengine nasikia wanatamani mpaka kuku!:-(
Ngojea wakamatwe tu na kuondolewa katika jamii.