Showing posts with label Kepteni Komba. Show all posts
Showing posts with label Kepteni Komba. Show all posts

Saturday, February 28, 2015

Historia Fupi ya Marehemu Captain Komba!

 Mbunge wa Mbinga na Msanii maarufu, Captain John Komba, alifariki dunia leo katika hospitali ya TMJ mjini Dar es Salaam, kutokana na athari za ugonjwa wa kisukari. Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
The late Captain John Komba


Historia Fupi ya Marehemu John Komba
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1954 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.


**********************************************************************

Waziri wa Ardhi,William Lukuvi (wa kwanza kushoto) akimfariji mke wa marehemu, Salome Komba

Khadija Kopa akilia kwa Uchungu nyumbani kwa Komba.
 

Captain John Komba Afariki Dunia

 Wadau, Mh. Captain John Komba, Mbunge wa Mbinga amefariki leo katika hospitali ya TMJ. Wanasema alikuwa anasumbuliwa na kisukari (diabetes).

Lazima niseme kuwa nakumbuka marehemu Captain Komba alivyoaanza kupanda chati. Alikuwa Sargent wa Jeshi na alikuwa anaimba katika kikundi cha wasanii. Alimwimbia Mwalimu ule wimbo wa 'We Love Freedom'.  Nimesahau ilikuwa sherehe ya nini. Mwalimu na wote tuliyokwepo tuliblow!  Alipata U-Captain haraka sana na mambo ya TOT ni ya kihistoria.

REST IN PEACE CAPTAIN KOMBA!

Kutoka Twitter:

Rest in peace, Tanzanian singer/politician Captain John Komba. I remember his rise to fame. 
Chama Cha Mapinduzi @ccm_tanzania 7m7 minutes ago
TANZIA:Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar.
0 replies10 retweets0 favorites Reply
Retweeted10



Kutoka EATV
 
East Africa TV
@ eastafricatv
1m
#TANZIA Mbunge wa Mbinga Magharibi
Kapt. John Komba amefariki dunia leo
saa 10 jioni katika hospitali ya TMJ
DSM kwa tatizo la Kisukari