Wadau, leo sherehe za Arobaini ya marehemu baba yangu mzazi, Dr. Aleck. H. Che-Mponda, zilifanyika mjini Dar es Salaam, pale nyumbani Tenki Bovu, Mbezi Beach Juu. Nafurahi mwanangu, Camara aliweza kuhdhuria pamoja na mdogo wangu Jessica.
REST IN ETERNAL PEACE DR. ALECK H. CHE-MPONDA (1935-2015)
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia
kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika
ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5
Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais
ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na
shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi
wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi ,
mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa
wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha
kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya
kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela
ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi
binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika
na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata
maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza
kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee
Mandela mahali pema peponi".
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo
tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.
Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote
zipepee nusu mlingoti.
I worked for Tanzania's Daily News for 11 years leaving as a Senior Reporter. I love acting, films, short story writing and cooking. I blog in English and Swahili. I am a member of the Screen Actors Guild (SAG) and AFTRA.
You can contact me at chemiche3@yahoo.com.