Showing posts with label Mzee Kipara. Ugonjwa. Show all posts
Showing posts with label Mzee Kipara. Ugonjwa. Show all posts

Monday, October 10, 2011

Hali ya Dr. Harrison Mwakyembe ni Mbaya! Amepelekwa India kwa Matibabu

Kutoka IPPMEDIA.Com

Dr Mwakyembe leaves for medical checkup in India

By Correspondent


10th October 2011

Works deputy minister Dr Harrison Mwakyembe has been rushed to India for treatment of a skin related disease.

Dr Mwakyembe, who is also Member of Parliament for Kyela, left the country yesterday morning accompanied by his wife, Linah.

To see him off at the airport was Works minister Dr John Magufuli and other people, including the IPP Executive Chairman, Reginald Mengi.

The family spokesperson, Victor Mwambalaswa, said Dr Mwakyembe is suffering from a skin disease.

Speaking on the phone from his home to our sister paper Nipashe before he left, Dr Mwakyembe said that he was going to India for further medical checkup but did not disclose what he was suffering from.

He dismissed reports that he was seriously ill, stressing that he was not in bad condition.

For his part, Dr Mwakyembe’s personal assistant, Salum Nkambi said he has been receiving many calls from well-wishers seeking to know the condition of their lawmaker.

Nkambi said the health status of Dr Mwakyembe was not bad as reported in the media (not The Guardian).

Chama Cha Mapinduzi publicity secretary Nape Nnauye, who had driven the deputy minister to the airport, said Mwakyembe was flying to Mumbai, India where he will undergo medical checkup.

He said Dr Mwakyembe was not accompanied by a doctor because his condition was not bad.

President Jakaya Kikwete on Saturday saw Dr Mwakyembe at his residence at Kunduchi Beach in Dar es Salaam.

Water minister Prof Mark Mwandosya, who left the country in June for medical treatment in India was admitted at Applo Hospital where he is still undergoing treatment.

Prof Mwandosya started feeling unwell when he was attending the budget parliamentary session in Dodoma in June this year.
He was first rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) before being referred to India for specialised treatment.

On Saturday he spoke by phone to Radio One saying that his condition was improving.

********************


Dr. Harrison Mwakyembe
Dk Mwakyembe Mgonjwa

Saturday, 08 October 2011

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe

AVIMBA MWILI MZIMA, JK AMTEMBELEA

Na Mwandishi wetu

AFYA ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ni tete baada ya kuugua ugonjwa uliomsababisha kuvimba mwili wote.Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na yeye mwenyewe zinaeleza kuwa, alianza kuwashwa ngozi miezi mitatu iliyopita kabla ya hali kubadilika siku za karibuni na hatimaye kuvimba sehemu kubwa ya mwili wake.

Mwakyembe alilieleza gazeti hili jana kuwa, baada ya hali yake kubadilika alianza kupata matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam akiwa nyumbani kwake Kunduchi Beach.Akizungumza na gazeti hili kwa shida, Dk Mwakyembe alisema hajui chanzo cha ugonjwa huo wa ngozi, daktari wake ndiye anaweza kuelezea kwa usahihi.

“Ni kweli naumwa nipo nyumbani, hata sura yangu imebadilika. Sasa hivi namsubiri daktari wangu, nilisikia natakiwa kupelekwa India kwa matibabu, nasubiri kauli yake si mimi niamue,” alisema na kuongeza;

“Siwezi kusema nimelishwa sumu, ninachosema mimi nimevimba kweli mwili mzima naumwa kweli hapa nimelala na sijui umenipataje kwa simu kwa sababu huwa siiwashi muda huu una bahati kweli”.

Mke wa Dk Mwakyembe Mkewe Linah Mwakyembe alipozungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Jumapili, alisema kwa mujibu wa daktari wake, Dk mumewe anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis.

“Alianza kuugua muda mrefu kidogo, kama miezi mitatu iliyopita, hali hiyo ilikuwa inatokea na kupotea hadi sasa ambapo hali imekuwa mbaya zaidi,” alisema.

Alisema madaktari waliomfanyia uchunguzi kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho walitoa majibu tofauti na kuongeza kuwa wapo waliosema hali hiyo ilisababishwa na kisukari na mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kulikuwa na chembechembe za sumu katika damu yake.

“Baada ya ngozi yake kubadilika sana na hali kuwa mbaya, tulienda hospitali na madaktari walitupa majibu tofauti, wapo waliosema ni kisukari na kuna mwingine alisema kuna chembechembe za sumu,” alisema Linah na kufafanua kuwa daktari aliyedai hivyo hakuwapa maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa Linah, ngozi ya Dk Mwakyembe inawasha na inakuwa kama inatoa mba mwili mzima hadi kichwani.

Aliongeza kuwa daktari wake ameshauri ufanyike uchunguzi wa kina zaidi ili kujua kama atahitajika kupatiwa matibabu nje ya nchi.

“Walipendekeza afanyiwe uchunguzi zaidi, hivyo kama kutakuwa na ulazima wa kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi basi watatueleza,” alisema Linah.

Alisema kuwa leo ndio watapata jibu kama atahitajika kwenda nje au kuendelea na matibabu hapa nchini.

Alisema kumekuwa na uvumi mwingi juu ya ugonjwa wa Dk Mwakyembe na kusisitiza kuwa wao kama familia wanasikiliza kinachosemwa na madaktari na kile watakachoshauri.

“Sisi tunaendelea kusubiri kile kitakachogundulika baada ya uchunguzi huo na kama kutakuwa na mengine tutajulishwa na kujua hatua itakayofuata,” alisema Linah.

Exfoliative Dermatitis Kwa mujibu wa maelezo ya kitabibu, ugonjwa huu huweza kusababisha madhara makubwa ya mwili na matatizo mengine hivyo kuhitaji uangalizi wa karibu wa kitabibu.

Ugonjwa huu ukikomaa husababisha ngozi ‘kuwaka moto’ na huathiri wanawake na wanaume lakini zaidi wanaume wenye umri kuanzia miaka 55.

Dalili Dalili za ugonjwa huu ni kuwashwa, mwili kuishiwa nguvu pia sehemu ya juu ya ngozi hupukutika.

Chanzo kwa mujibu wa maelezo ya kitabibu, sababu za ugonjwa huo bado hajizulikani, hata hivyo matukio ya ugonjwa huu mara nyingi yanahusishwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi, madhara ya dawa kama penicillin, sulfonamides, isoniazid na phenytion.

Rais Kikwete amtembelea Baadaye mchana Rais Jakaya Kikwete alifika nyumbani kwa Dk Mwakyembe Kunduchi Beach kumjulia hali.

Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela mwaka 2008, aliongoza Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Mkataba wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond.

Katika baraza jipya la mawaziri ambalo Rais Kikwete aliliunda mwaka jana, alimteua Dk Mwakyembe kuwa Naibu waziri wa Ujenzi akimsaidia Dk John Magufuli.

Mikasa ya Mwakyembe

Mei 21 mwaka 2009 Dk Mwakyembe alinusurika kufa katika ajali mbaya ya gari eneo la Ihemi kilomita 40 kutoka Iringa mjini akiwa safari kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, gari alilokuwa akisafiria Toyota Landcruiser T362ACH, liliacha njia saa moja asubuhi baada ya kukanyaga shimo na tairi ya upande wa kulia kuchomoka na dereva wake, Joseph Msuya (30), kupoteza mwelekeo kabla ya gari hilo kutoka nje ya barabara upande wa kushoto na kuparamia mti kisha kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk Mwakyembe akijaribu kulipita lori kabla ya kukanyaga shimo hilo.

Dk Mwakyembe na abiria wengine waliokolewa na Wasamaria wema pamoja na trafiki wawili waliokuwa kwenye basi dogo wakisafiri kutoka Iringa kwenda Njombe.

Baada ya ajali hiyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Ilifahamika kuwa aliumia taya kisha alihamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) aliunda tume iliyoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati huo, Kamanda James Kombe, kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Matokeo yalionesha kwamba ilisababishwa na uzembe wa dereva wake, Msuya.

Tuesday, September 06, 2011

Mzee Kipara Yu Hoi Anahitaji Msaada!

(Mzee Kipara akijaribu kusimama)
(Mzee Kipara Majuzi akijaribu kutoka kitandani)(Mzee Kipara Mwaka 2007 Akipelekwa nyumbani baada ya kushuti Scenes zake katika Sinema, Bongoland II, katika sinema hiyo aliigiza kama Imam)

Wadau, sielewi nchi yetu Tanzania! Mzee Kipara aka. Mzee Fundi Saidi ni nyota na mkongwe katika sanaa za maigizo Tanzania. Lakini ona anavyoteseka na kuishi maisha ya dhiki! Wasanii wengi wa Tanzania wanaishia kuishi maisha ya dhiki na kusahauliwa kabisa!


Someni Malalamiko ya Mzee Kipara kwa KUBOFYA HAPA:


****************************************************************************
Kutoka Fundi wa Kombo Blog http://fundirkombo.blogspot.com/

Napenda nitoe masikitiko yangu kwa wasanii wa Sanaa ya Maigizo wote Nchini kwa kutoonyesha msimamo wa pamoja ili kuweza kumsaidia Mzee wetu Mzee Kipara (Fundi Said) ambaye kwa sasa ana afya ambayo sio nzuri pamoja na uzee lakini hali ngumu ya kimaisha ndio inayochangia zaidi.

Mzee Kipara ni msanii wa muda mrefu sana katika Tasnia hii ya sanaa ya Uigizaji, ni muigizaji mkongwe sana katika Taifa letu, kwa wale wasiomjua alianza kuigiza sanaa toka mnamo mwa miaka ya 1964 enzi za RTD (Redio Tanzania) kwa sasa TBC hii kwa faida ya vizazi vya sasa msio fahamu hili.

Baadae Mzee kipara walianzisha kikundi cha maigizo ambacho kikawa kinarushwa na TV ya ITV ambacho amedumu nacho kwa muda mrefu sana kikiitwa Kaole. Katika kipindi chote hiki cha Kaole aliwafundisha wasanii wengi sana ambao kwa sasa wengi mnawasikia au mnaziona kazi zao kwenye Luninga zenu.

Cha kunisikitisha wengi wao hawajaonyesha upendo wao hata kidogo kwa mzee huyu, nitakua mnyimi wa Fadhila kama sita mshukuru sana Stephen Kanumba nakumbuka alikua msanii wa kwanza kwanza kwenda kumsaidia huyu Mzee; namshukuru sana, najua wapo wengine ambao pia walikwenda kwa nyakati tofauti tofauti kuweza kumuona huyu mzee au hata kumsaidia kwa chochote kile.

Mimi binafsi kama mwakilishi wa KAPINGAZ Blog napenda kuwashukuru wote waliofanya hivyo, ila ombi langu kwenu ninyi wasanii wa sanaa ya Maigizo ni kwa nini msiandae tamasha lolote ambalo mnaweza mkakusanya kiasi kikubwa cha fedha kikaweza kumsaidia huyu Mzee wenu badala ya kwenda mmoja mmoja kumuona huyu Mzee, kumbukeni na nyie ni vijana kwa leo itafika wakati mtazeeka kama huyu mzee na watatokea wengine mmewafundisha hiyo sanaa naamini na nyie mnaweza mkasikitika kama mzee huyu.

Naomba niwape mfano wa Dada Asha Baraka, Mkurugenzi wa African Star (Twanga Pepeta) nampongeza sana huyu dada aliweza kuandaa tamasha la Dansi kwa ajili ya kukusanya michango ya kumsaidia Mzee Muhidin Ngurumo ili aweze kupata matibabu vizuri, na mpaka leo naandika masikitiko yangu, Mzee Ngurumo leo anapanda kwenye stage kuimba na wenzie katka tamasha la sikukuu ya Idd el Fitr.

Nawaomba wasanii wote katika sanaa ya maigizo muweze kulitazama hili la Mzee Kipara kama ni jambo lenu wote, na hata mnapokua mnakwenda kwenye vikao vyenu na BASATA muweze kuliongelea hili, ili muweze kua na umoja wenye nguvu wa kuweza kusaidiana kwenye matatizo kama haya. Tunawaona mara kwa mara mnaenda kufanya shughuli mbali mbali sehemu tofauti, hasa za kujipongeza katika mafanikio flani ni vema mnapokua huko mkumbushane la mzee huyu msimuache aishi maisha haya ni aibu kwenu wasanii wote hasa zaidi nyie mliopitia Kaole.

Naomba wana Blog wenzangu tushirikiane katika hili. Asante

************************************************************

Kama Unataka kuchangia Mzee Kipara tafadhali tembelea Blogu ya Kaka Michuzi:
au BOFYA HAPA