Showing posts with label Northampton. Show all posts
Showing posts with label Northampton. Show all posts

Saturday, April 08, 2017

Uzinduzi wa WASATU - Northampton, Uingereza

PICHA ZA HABARI : UZINDUZI WA WASATU NORTHAMPTON , UINGEREZA

Na Freddy Macha 

 Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na  wenzao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro.
 

WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya. Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa walio Northampton; kwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania. 

Pichani: Watanzania na wasanii wenzao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton