Showing posts with label Nuru Mkeremi. Show all posts
Showing posts with label Nuru Mkeremi. Show all posts

Monday, August 25, 2008

Da Nuru Mkeremi akumbuka Wagonjwa wa Kansa Tanzania


Hivi karibuni, Dada Nuru Mkeremi alifiwa na Mama yake mzazi Mama Nellie Kidela, ambaye alikuwa mtangazaji miaka mingi Radio Tanzania. Dada Nelie aliugua kansa ya ziwa muda mrefu. Alifariki mwaka jana mjini Dar es Salaam. Rest in Peace.

Juzi Da Nuru alituma huo ujumbe kwa marafiki zake
.

********************************************************************

Hi yall, I was comforted when I heard that my mom was surrounded by people of God when she was on her dying days........It still hurts, don't get me wrong.

This morning I remembered all those cancer patients at Ocean Road Hospital who have been referred from other hospitals............who is there to comfort them? Who is there to cry with them? How many people really pray for them and their families? I just mentioned Ocean Road hospital to represent all other hospitals.

I guess I was called for this, I ask my friends for supports both spiritually and materially. I do this in honor of all those who were there for my mom. God bless you all mightly in Jesus name!!Amen

Tuesday, January 15, 2008

Remembering Nellie Kidela 1946-2007

Mtoto wa marehemu Nellie Kidela, Nuru Mkeremi, kaburini mwa mama yake (Oct. 24, 2007).

Nellie Kidela (wa pili kutoka kushoto) na familia yake June, 2007


Nuru Mkeremi akipewa rambirambi kutoka mwakilishi wa TAMWA, Ichikaeli Maro. Hapo ni kwenye mazishi ya Dada Nellie October 12, 2007.

Dada Nellie akiwa na Violet Weinberg, ambaye alikuwa mpigania uhuru wa African National Congress, January 11, 1981.

Dada Nellie Kidela, alifariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana 2007. Alikuwa ni mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) miaka mingi. Mwanae, Nuru Mkeremi wa Boston ameniletea picha na habari zaizi nizi - share na wadau.

Nellie Kidela, alijuinga na RTD 1976 kama mtangazaji (radio broadcaster). Aliwahi pia kuwa mwalimu katika shule za msingi za Oyster Bay na Olympio mjini Dar es Salaam.

Alivyokuwa RTD alifanya kazi katika Idhaa za Kiswahili na ya kiingereza (External Service). Aliandaa vipindi kama Face the Mike, Ugua Pole, Chei Chei Shangazi, From Me to You, Potpourri, Songs to Remember, na Majira.

Alikuwa Mwanachama wa Amnesty International, Tanzania. na alifanya kazi nao kila akipata nafasi.

Dada Nellie ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha waandishi wa habari wanawakeTanzania (TAMWA). Mkutano wa kwanza kabisa ulifanyika nyumbani kwa Dada Nellie.

Miaka ya 80, Dada Nellie alihusika sasa na chama cha Tanzania Cerebral Palsy and Mental Retardation. Alikuwa na mtoto ambaye aliugua na kuathirika na Cerebral Palsy akiwa na miaka 6. Mtoto alifariki miaka ya 90.

Mwaka 1999, Dada Nellie, alikuja kumtembelea mwanae Boston. Ndo hapo alienda hospitali na waligundua anaumwa kansa ya ziwa. Alipata matibabu Boston University Medical Center. Baada ya matibabu walidhania amepona. Alikaa miaka sita katika 'remission'. Kansa ilivyorudi mwaka juzi walikuta umeingia kwenye mifupa.

Dada Nellie alijitahidi sana kuendelea na shughuli zake, japo alikuwa na maumivu makali sana shauri ya kansa.

Dada Nuru anasema mama yake alivyofariki alikuwa anatabasamu. Kabla hajakata roho aliwaambia watu kuwa wasiwe na wasiwasi atakuwa okay.

Dada Nellie atakumbukwa daima na familia, marafiki, na wasikilizaji wa Radio Tanzania Dar es Salaam.

REST IN PEACE

Saturday, October 13, 2007

Mwandishi wa Habari Nellie Kidela amefariki dunia.

Leo nimepata habari kuwa mwandishi wa habari na mtangazaji wa siku nyingi wa Radio Tanzania Dar es Salaam, Nellie Kidela, amefariki dunia.

Dada Nelly ni moja wa waanzilishi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, TAMWA. Mkutano wa kwanza kabisa ulifanyika nyumbani kwake.

Taarifa niliyonayo ni kuwa Dada Nellie alifariki siku ya Jumatatu tarehe nane Oktoba na alizikwa, jumatano tarehe 10 Oktoba katika makaburi ya Kinondoni. Alikuwa ameugua ugonjwa wa kansa siku nyingi. Na miaka ya nyuma aliwahi kupata matibabu hapa Boston.

Dada Nellie alikuwa mama yake mzazi na Nuru Mkeremi wa hapa Boston, Massachusetts.

Mungu ailaze roho take mahali pema mbinguni. AMEN.