Showing posts with label Nzi. Show all posts
Showing posts with label Nzi. Show all posts

Thursday, June 18, 2009

Rais Obama aua Nzi! PETA waja juu!


Sasa jamani hao watu wa PETA (People for the Ethical Treatment of Animals) wamezidi. PETA ni kikundi kinachotetea haki za wanyama.

Ni hivi, jana Rais Obama alikuwa anahojiwa na CNBC. Nzi alikuwa anamsumbua. Aliomba wasimamisha interview halafu kamwua nzi aliyetua kwenye suti yake. Watu wengi walimsifia kwa jinsi alivyomwua nzi, lakini PETA wanasema ni bora huyo nzi angekamtwa na kuachiwa huru nje. Jamani!

Duniani kuna mabilioni ya nzi! Nzi ni mdudu mchafu anasambaza magonjwa. Kwangu nzi hana haki na mimi nawaua bila huruma kila nikipata nafasi!
HEKO RAIS OBAMA!
Kwa habari zaidi someni: