Thursday, June 18, 2009

Rais Obama aua Nzi! PETA waja juu!


Sasa jamani hao watu wa PETA (People for the Ethical Treatment of Animals) wamezidi. PETA ni kikundi kinachotetea haki za wanyama.

Ni hivi, jana Rais Obama alikuwa anahojiwa na CNBC. Nzi alikuwa anamsumbua. Aliomba wasimamisha interview halafu kamwua nzi aliyetua kwenye suti yake. Watu wengi walimsifia kwa jinsi alivyomwua nzi, lakini PETA wanasema ni bora huyo nzi angekamtwa na kuachiwa huru nje. Jamani!

Duniani kuna mabilioni ya nzi! Nzi ni mdudu mchafu anasambaza magonjwa. Kwangu nzi hana haki na mimi nawaua bila huruma kila nikipata nafasi!
HEKO RAIS OBAMA!
Kwa habari zaidi someni:


6 comments:

Anonymous said...

Mimi niko tayari kusafirisha nzi wote Tanzania na kuwapeleka ofisni kwa hao washenzi wa PETA! Wamezidi!

Fadhy Mtanga said...

Vyama vingine! Akili zao haziwatoshi.

chib said...

Inashangaza, mimi nafikiri basi tuanze kutetea na virusi vya mafua ya nguruwe, maana navyo ni viumbe hai.

Anonymous said...

sasa si wawafuge majumbani mwao halafu waone kilichomtoa kanga manyoa! wataharisha kama ngisi halafu wakipona hapo waendeleze libeneke la kutetea huo uchafu!

Mkongwe said...

Ndo maana wanasema MAJUU HAMNAZO!

Watu haohao wanakula vyakula mbali mbali bila kuzingatia kuwa vimetokana na 'kuuwawa' kwa mimea/wanyama. Mbona hawadai haki ya mimea kuishi?

Anonymous said...

Next PETA will defend mosquitoes!