Uchumi wa Anguilla unategemea utalii tena utalii wa hali ya juu, yaani High Class. Nilipita uwanja wa ndege wao jana na nikaona private jets tano zimeegeshwa. Matajiri na mastaa wengi wanakuja hapa maana hakuna usumbufu kama Jamaica, Bahamas, Barbados nk.
Ila ukienda dukani kila kitu ni imported, utadhani uko supermarkt USA. Niliona kagenge walikuwa wanauza ndizi, viazi na vitunguu tu. Ardhi hapa haina rutuba imejaa mawe na mchanga, lakini wana beach nzuri sana, mchanga laini, halafu mweupe!
Sehemu nyingi ziliharibiwa na kimbunga kilichopita.