Showing posts with label Anguilla. Show all posts
Showing posts with label Anguilla. Show all posts

Thursday, September 02, 2010

Hurricane Earl Kilivyopiga Kisiwa cha Anguilla

Hurricane Earl kilipita nchini Anguilla mwanzoni mwa wiki hii. Kwa siku kadhaa visiwa vya Leeward Islands vilikosa umeme. Kwa bahati nzuri hakuna aliyepoteza maisha kutokana na kimbunga. Ila nyumba kadhaa zilipoteza paa zao na zingine kuaathirika kwa upepo kali na kuangukiwa na miti. Mnaweza kusoma habari zaidi HAPA:

Hivi sasa hapa Massachusetts tuko chini ya Hurricane Watch.
Mdogo wangu Malaika Che-Mponda ambaye anakaa huko ameniletea picha hizi.





Baada ya Kimbunga Earl Kupita


Paa ilitoka kwenye Stadium yao
Miti imeanguka
Hizo boti zitatembea tena kweli?
Mwenye boti kapata hasara!
Barabara ulizibwa


Jamaa aliamua kuacha ferry baharini...ilipona!

Sunday, August 08, 2010

Safari ya Anguilla Katika Picha 2

Blowing Point Beach. Beach zote za Anguilla ziko wazi kwa kila mtu, hata kama kuna hoteli ya kifahari. Lazima waruhusu watu kwenda bila kiingilio.

Hapa nakata tiketi ya kupanda boti kwenda kwenye uwanja wa ndege St. Maarten ili nipande ndege ya kwenda Boston.
Kimbunga ikikaribia Anguilla.
Hiyo ferry ilienda St. Maarten ingawa kulikuwa na mawingu na dalili ya kimbunga. Lazima baadhi ya walikuwemo walitapika shauri ya mawimbi makali.
Mimi na baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda nje ya ofisi ya Uhamiaji ya Anguilla. Ndani Air Condition safi, na huduma nzuri.
Nikienda kupanda ferry kwenda st. Maarten.
Niko kwenye ferry.
Hapa niko Beach nikijiandaa kwenda snorkeling. Niliona samakai wazuri kweli, wenye marangi rangi. Tena walikuwa karibu na ufukwe.

Thursday, August 05, 2010

Anguilla Festival 2010


Mshindi akijiandaa kuimba wimbo wake kuhusu umoja wa visiwa vya Caribbean.
Mshindi akiimba wimbo wake.
"YAH MAN! Anguilla kuzuri!"
Mashindano ya Calypson ya Vijana kwenye TV. Huyo binti hakuwa na sauti nzuri lakini nilipenda hiyo nguo aliyovaa ya kuwakilisha Anguilla.
Waziri Mkuu (Chief Minister) wa Anguilla Hubert Hughes

Wadau, jana jioni nilienda kwenye mashindano ya Calypso hapa Anguilla. Ilikuwa safi sana. Walishindana wanawake wanne na wnanauma 6. Mwanamke ndiye alishinda na nyimbo yake ya kuhusu visiwa vya Caribbean kuwa na umoja.

Nyimbo nyingi zilihusu siasa za Anguilla. Nimeshangaa maneno wazi wazi hakuna maficho. Mfano walisema kuna rushwa tele, waAnguilla wanaonewa na mabenki. Hawawezi kupata mikopo. Walilamika kuwa waChina wana haki kuliko waAnguilla na sasa wana maduka makubwa ya Hardware na restaurants tele.

Mwanamke fulani aliimba nyimbo kuhusu kupujunwa uroda na mume wake. Nimempenda jamaa 'Springer' ambaye ni jirani yetu hapa Blowing Point. Aliimba wimbo ambayo ilisema aliweza kutabiri kuwa kutakuwa na amani dunia nzima siku moja.

Lakini ajabu, jamaa fulani aliimba nyimbo kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni hapa kisiwani. Walitoa bango ya waziri mkuu na kuitumia katika wimbo! Nilishutuka, nikamwuliza mtu aliyekaa karibu na mimi ni nani huyo? Khaa! Jamani, kumbe nilikaa naye kwenye ferry kutoka Anguilla. Nilijua ni mtu wa maana jinsi watu walivyouwa wanamsalimia, lakini sikujua kamani waziri mkuu! Hakuwa na mbwembwe zile kama Bongo, mkubwa kubebewa begi, walinzi kibao, nk. Tena aliniomba kuazima kalamu kwa ajili ya kujaza fomu ya uhamiaji, lakini mtu mwingine alikuwa ameaimza. Yeye ndo alikuja kakaa na mimi na tulikuwa tunaongea, na nilitaka kumwuliza kama ana ndugu a shemeji yangu lakini sikumwuliza. Nadhani alijua mimi sikumtambua.

Habari zaidi baadaye.

Mnaweza kusoma habari za Anguilla Festival 2010 hapa:

http://www.axasummerfestival.com/results.php?eventID=24

Wednesday, August 04, 2010

Anguilla Safari Katika Picha I

Kisiwa cha Anguilla kinavyoonekana kutoka angani.

Kisiwa cha St. Maarten. Tulikuwa karibu kutua uwanja wa ndege. Njia rahisi kwenda Anguilla ni kupanda ndege hadi St. Maarten halafu unapanda boti/ferry kwenda Anguilla.
Mama Mkwe wa mdogo wangu, mimi, na Eustace. Tuliekuwa tumetoka dukani. Tulisimama kwenye kivuli cha klabu bubu. Wanauza nyama choma hapo lakini walikuwa wamefunga kwa ajili ya sikukuu.
Kisiwa cha St. Maarten kwa mbali. Hapa nilipofikia ni eneo la Blowing Point, Anguilla.
Baba yangu, Dr. Aleck Che-Mponda akipunga hewa na mjukuu wake, mpwa wangu Anguilla.
Shule ya msingi ya eneo ya eneo la South Hill, Anguilla. Ina mafeni na Air conditioning!
Hapa ni eneo la shule ya msingi. Huwezi kwenda mwendo wa kasi maana kuna matuta kila baada ya mita 20! Wanajali sana usalama wa watoto wao.
Mama akisubiri kumwona daktari. Huduma pale ni nzuri sana.
Nje ya zahanati. Mama yangu alikuwa anajisikia vibaya tukampeleka kwenye zahanati. Daktari pale ni MNigeria.
Huyo Rastaman katika kisiwa cha St. Maarten. Anasema anakwenda Anguilla kutembea kila wikiendi. Alikuwa mcheshi kweli.
Hapa napumzika kwenye veranda ya nyumba ya shemeji yangu. Huyo mbwa 'Zoe' alikuwa ananiamsha kila nikitaka kusinzia. Upepo mzuri kweli kutoka kwenye Caribbean Sea. Kwa mbali mnaweza kuon kisiwa cha St. Maarten.

Tuesday, August 03, 2010

Kimbunga Anguilla

Hivi sasa tunapigwa na storm hapa Anguilla. Usafiri mkuu kati ya kisiwa cha St. Maarten na Anguilla ni maboti/ferry. Walizisimamisha kwa muda. Lakini naona sasa zimeanza kutembea. Mbwa walianza kuchimba mashimo, watu wakahofia kuwa kimbunga kitakuwa kali sana. Naona bahari inapoa sasa. Mawimbi yalikuwa makali sana. Picha nitabandika hivi karinuni.

Saturday, July 31, 2010

Safarini Anguilla

Wadau, niko nchini Anguilla, kwa mdogo wangu Malaika. Nitaposti habari za Anguilla hivi karibuni.

Sunday, February 08, 2009

Anguilla Katika Picha

Nilipiga picha hii nikiwa kwenye ferry. Anguilla haina milima mirefu! Kutoka angani inaonekana fleti kama imepigwa pasi.
Barabara ya kuelekea kwenye hoteli ya fahari (5Star) Cap Juluca. Kwa mbali unaweza kuona kisiwa cha St. Maarten

Ukihitaji maji unaletewa. Ukitaka tanki nzima ni dola $500! Watu wengi wanakinga maji ya mvua.

Mbuzi wa Anguilla ( Waingereza waliabika mwaka 1969 walipovamia Anguilla na kukutana wa wafuga mbuzi badala ya wapiganaji)

Mzungu akijipika juani! Wazungu huko wameungua na jua, wengine wekenduuu! Kwa nini wanataka kuwa weusi halafu wanadharau watu weusi?
Anguilla Health Authority

Huyo Rasta Man anamtungia huyo Bi Kizee wimbo hapohapo. Huyo Bi Kizee anaitwa Nancy na ilikuwa party ya kusherekea Birthday yake....ana miaka 75. Rum punch zilikuwa zimenikolea lakini wimbo ulisema kitu kama, Nancy is so beautiful but she got ugly man.

Usikojoe hadharani!

Boti inajengwa kwa ajili ya mashindano ya mashua. Kushindana mashua ni mchezo mkuu wa Anguilla.
Barabara za Anguilla ni nzuri hazina mashimo. Kwa vile ni kisiwa kadogo, hakuna barabara enye njia zaidi ya mbili. Niliamua kuingia kwenye maji, lakini yalikuwa baridiii! Mchanga kwenye beach zao ni mweupe halafu laini kama unga!
Hapa ni Blowing Point Beach
Ferry iliyonipeleka uwanja wa ndege St. Maarten. Ukitaka kwenda Anguilla inabidi uende kwenye kisiwa jirani cha St. Maarten ambayo iko chini ya waHolanzi na waFaransa. Anguilla ni koloni ya Uingereza.

Ndege wa Taifa wa Anguilla ni Turtle Dove
Jogoo akitamba Anguilla

Watoto wa shule huko wanachukuliwa na School Bus, huduma ya school bus inalipiwa na serikali

Nyumba asili ya Anguilla. Nilibishana na watu huko kuhusu hizo nyumba, walisema eti nyumba asili (huts) za waafrika ni ndogo zaidi. Nikwaambia nyumba zao asili ni ndogo kweli!

Nyumba ya James Ronald Webster ambaye anaitwa mkombozi wa Anguilla. Bwana Webster aliongoza mapinduzi huko mwaka 1967. Mwaka 1969 waingereza walipavamia na walipokelewa kwa shangwe na wenyeji.