Nimeona hizi picha kwa Michuzi Jr. (Jiachie Blog). Huyo mshiriki wa Miss Utalii alikuwa kwenye ziara. Ghafla alianguka. Wanasema kuwa harufu ya dawa wanazotumia kiwandani zilimwangusha. Inawezekana. Ila navyofahamu hizi pageant za urembo, mara nyingi mtu akianguka hivyo ni shauri ya njaa. Hao wagombea wanakula kidogo sana au hawali kabisa kusudi wakonde au wabakie wembamba. Wakati mwingine wanapata dehydration (ukosefu wa maji mwilini) na utapiamlo. Inatokea sana kwenye pageant za Marekani. Lakini kwa Bongo huenda ana malaria. Pole sana Sara Salum.
Mshiriki wa miss utalii 2008 Sara Salum kutoka Dodoma akipewa sapoti ya kutembea na baadhi ya wasimamizi wa walimbwende hao waliofika kushuhudia kazi za uchapaji ndani ya kiwanda cha Image Printer,kilichopo Nyerere road jijini dar.

Moja ya washiriki wa miss Utalii Tanzania 2008, Sara Salum 25, Dodoma alidondoka katika ziara ya kutembelea kiwanda cha Image Printer leo mchana baada ya kuzidiwa na kemikali zinazotumika katika masuala ya uchapaji kiwandani hapo.
(Picha kutoka Michuzi Jr. Blog)