
Jamani, hizi siku za karibuni kumekuwa na joto kweli hapa Marekani. Sehemu zingine joto ni kupita 100Degrees Farenheit! Rais na familia yake wako likizo. Kesho nadhani watafika hapa Massachusetts. Watakuwa Martha's Vineyard. Mke wa Rais amezua zozo, eti hatakiwi kuvaa kaptura. Mimi nasema kwa nini asivae? Si wako likizo, siyo kwenye ziara rasmi. Hapa watu wanatembea karibu uchi, na kuvaa vinyuzi wakisema eti nguo! Hebu wamwache mama wa watu afaidi likizo yake! Au wanamwonea wivu miguu yake mizuri?
Mnaweza kusoma habari zaidi:


