Thursday, August 20, 2009

Michelle Obama Avaa Kaptura na Kuzua Zozo!


Jamani, hizi siku za karibuni kumekuwa na joto kweli hapa Marekani. Sehemu zingine joto ni kupita 100Degrees Farenheit! Rais na familia yake wako likizo. Kesho nadhani watafika hapa Massachusetts. Watakuwa Martha's Vineyard. Mke wa Rais amezua zozo, eti hatakiwi kuvaa kaptura. Mimi nasema kwa nini asivae? Si wako likizo, siyo kwenye ziara rasmi. Hapa watu wanatembea karibu uchi, na kuvaa vinyuzi wakisema eti nguo! Hebu wamwache mama wa watu afaidi likizo yake! Au wanamwonea wivu miguu yake mizuri?
Mnaweza kusoma habari zaidi:

6 comments:

Anonymous said...

acha kutetea pumba.
hao wanaovaa vichupi nani anawajua,nani anawaongelea,wana nafasi gani katika jamii, kwa nafasi ya Michelle hakustahiri kuvaa hivyo.
think twice

Anonymous said...

Wana Wivu!

Anonymous said...

Ana miguu mizuri. Sielewi watu wanalalamika nini. Wazungu wanatembea karibu uchi kukiwa na joto halafu wanamsema mtu aliye vaa vizuri kiasi.

Anonymous said...

u guys think twice hivi michelle angekuwa mtu wa kawaida tu yaani kama mimi na wewe unadhani hii ingekuwa ishu. imekuwa issue coz yeye ni first lady so haipendezi kwa nafasi yake kuvaa hivyo

Anonymous said...

hayuko uchi so she is ok

Anonymous said...

Ukishakuwa kwenye uongozi lazima uelewe kuwa kila utakalolifanya litafuatiliwa kwa karibu hivyo ni vyema ukajitaidi kufanya yale yaliyo mazuri ili uwe mfano wa kuigwa. Kuvaa vichupi na vikaptura vifupi kwa mke wa Rais haipendezi ingawa yeye binafsi (Michelle) angependa kila fashion isimpite. Hizo ndo gharama za kuwa kwenye uongozi....uhuru wa kufanya mambo binafsi unapungua!