Kunbe Cold War haijaisha. Wadau, mbavu sina. Tangu jana jioni habari kubwa hapa Boston ni kuwa mashushushu kutoka Urusi wamekamatwa Cambridge. Watu wanashangaa. Walikuwa wanaishi kama mke na mume na eti walionekana kama watu wa kawaida. Of course walikuwa wazungu! Mwanamke eti alikuwa mrembo kweli mwenye nywele blonde! Mnaweza kuona picha yake HAPA. Kwenye taarifa ya habari wakati wa editorial wakiwaongelea, waliweka na muziki wa sinema za James Bond.
Kinachoniudhi ni kuwa kama wewe ni mweusi na unakaa Cambridge hao jirani zako wa kizungu wantakufanyia background check! Ukipita kwenye mitaa kadhaa wanaita polisi maana wanadhani mwizi au una nia mbaya! Kuna siku mimi na marehemu mume wangu tulikuwa tunatembea kwa mguu kwenye mtaa fulani. Nyumba ilikuwa inauzwa tukasimama mbele na kuliangalia. Tukaendelea na safari, si tulifuatwa na mzungu na kuulizwa maswali ya jela. Aliona aibu alipogundua kuwa tulikuwa jirani zake.
Anyway, nirudi kwa hao waRusi. Hao kwa vile walikuwa wazungu hakuna anayesema kitu. Ndo FBI wameshutua watu jana kusema hao walikuwa mashushushu! Na mimi ningesema si hao tu, wako na wengine. Walikuwa wanavizia wasomi wa Harvard na MIT. walikuwa wankaa nyumba fulani enye rangi ya njano huko Trowbridge St. karibu na Harvard Square na Cambridge Rindge & Latin High School.
Wanasema kuwa nia ya hao mashushushu ilikuwa kuishi kama waMarekani na kujuana na watu wenye uhusiano na siasa na mambo ya kitaaluma. Habari walizokuwa wanapata eti walikuwa wanatuma Urusi katika picha.
Mbinu waliotumia ni kukaa nyumba ambayo wanakaa wanafunzi. Wanafunzi wamahama hama hivyo watu jirani wanaokaa muda mrefu katika eneo hawapati nafasi ya kuwajua, na ukiwaona una sema wanafunzi tu.
Haya wazungu hebu acheni kushuku kila mweusi kuwa ni mbaya, wacheki na wazungu wenzenu! Tumechoka!
Kwa habari zaidi someni:
http://www.foxnews.com/us/2010/06/29/authorities-arrest-alleged-russian-spies-massachusetts/
http://www.cnn.com/2010/CRIME/06/29/russian.spying.arrests/?hpt=T2
http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2010/06/29/AR2010062902062.html
Showing posts with label Spy. Show all posts
Showing posts with label Spy. Show all posts
Tuesday, June 29, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)