Tuesday, June 29, 2010

Mashushushu wa KiRusi wakamatwa kwetu Cambridge

Kunbe Cold War haijaisha. Wadau, mbavu sina. Tangu jana jioni habari kubwa hapa Boston ni kuwa mashushushu kutoka Urusi wamekamatwa Cambridge. Watu wanashangaa. Walikuwa wanaishi kama mke na mume na eti walionekana kama watu wa kawaida. Of course walikuwa wazungu! Mwanamke eti alikuwa mrembo kweli mwenye nywele blonde! Mnaweza kuona picha yake HAPA. Kwenye taarifa ya habari wakati wa editorial wakiwaongelea, waliweka na muziki wa sinema za James Bond.

Kinachoniudhi ni kuwa kama wewe ni mweusi na unakaa Cambridge hao jirani zako wa kizungu wantakufanyia background check! Ukipita kwenye mitaa kadhaa wanaita polisi maana wanadhani mwizi au una nia mbaya! Kuna siku mimi na marehemu mume wangu tulikuwa tunatembea kwa mguu kwenye mtaa fulani. Nyumba ilikuwa inauzwa tukasimama mbele na kuliangalia. Tukaendelea na safari, si tulifuatwa na mzungu na kuulizwa maswali ya jela. Aliona aibu alipogundua kuwa tulikuwa jirani zake.

Anyway, nirudi kwa hao waRusi. Hao kwa vile walikuwa wazungu hakuna anayesema kitu. Ndo FBI wameshutua watu jana kusema hao walikuwa mashushushu! Na mimi ningesema si hao tu, wako na wengine. Walikuwa wanavizia wasomi wa Harvard na MIT. walikuwa wankaa nyumba fulani enye rangi ya njano huko Trowbridge St. karibu na Harvard Square na Cambridge Rindge & Latin High School.

Wanasema kuwa nia ya hao mashushushu ilikuwa kuishi kama waMarekani na kujuana na watu wenye uhusiano na siasa na mambo ya kitaaluma. Habari walizokuwa wanapata eti walikuwa wanatuma Urusi katika picha.

Mbinu waliotumia ni kukaa nyumba ambayo wanakaa wanafunzi. Wanafunzi wamahama hama hivyo watu jirani wanaokaa muda mrefu katika eneo hawapati nafasi ya kuwajua, na ukiwaona una sema wanafunzi tu.

Haya wazungu hebu acheni kushuku kila mweusi kuwa ni mbaya, wacheki na wazungu wenzenu! Tumechoka!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.foxnews.com/us/2010/06/29/authorities-arrest-alleged-russian-spies-massachusetts/

http://www.cnn.com/2010/CRIME/06/29/russian.spying.arrests/?hpt=T2

http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2010/06/29/AR2010062902062.html

4 comments:

Anonymous said...

Najua wazungu wabaguzi na kila kitu ila beef ulilonalo kwao ni kubwa.Punguza makali ya beef lako kwao Obama wanamkera lakini anawavumilia. Wazungu (Wagunzu) na Wanaume naona walikukosea sana wasamehe

Anonymous said...

Hao maspy wamejaa kibao Bongo! Wako kutoka Urusi, North Korea na China.Baada ya miaka 50, Tanzania itakuwa china ndogo.

Anonymous said...

he he he he hewee anonymous wa hapo juu unaonekana ww upo ka wale walamba miguu ya mzuungu hadi leo hii(mkoloni,kaburu)kwa taaarifa yako hamna mapenzi ya mzungu na mswaili never ukaee ukijua hilo kama unaona wanasaka ujamaa kwako ujuee kuna maslahi flani wanatarget kwako wakishaapata hao nduki.JAAAMI YENYE LAANA HIO MAKABURU


VIVA MUGABE
VIVA MALEMA JULIUS

Anonymous said...

Kwenu Cambridge? Nadhani kwenu ni Chalinze au Maneromango Cambridge ina wenyewe.