Showing posts with label Sumaye. Show all posts
Showing posts with label Sumaye. Show all posts

Tuesday, July 03, 2007

Wazazi Wangu safarini Boston

Kutoka Kushoto, Mhesimiwa Frederick Sumaye, Dr. Aleck Che-Mponda, mimi na mama yangu. Tulienda kumsalimia Mheshimwa Sumaye, ambaye kwa kweli alikuwa mkarimu sana. Msaidizi wake alitupikia mishikaki mitamu kama nyumbani. Mheshimiwa Sumaye amemaliza masomo yake Harvard University hivi karibuni.


Baba akiagana na Mheshimiwa Sumaye ambaye alikuwa jirani yangu hapa Cambridge, Ma. Ndo siku nilikabidhi kanda za sinema ya Tusamehe na Bongoland.

Baba na Mama wakiwa South Station, Boston Ma. kuelekea New York City ambapo walienda kusalimia ndugu na marafiki.


Dr. Aleck Che-Mponda akicheki sanamu ya mbwa aina ya St. Bernard huko Mohegan Sun.

Thursday, June 07, 2007

Mheshimiwa Sumaye Atoa Shukrani kwa WaTanzania New England



Mheshimiwa Sumaye na mke wake Esther wakifungua densi.

Leo aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka kumi, mheshimwa Frederick Sumaye, amemaliza masomo yake na kuhutimu shahada ya juu ya Masters of Public Administration kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, John F. Kennedy School of Government mjini Cambridge, Massachusetts, USA.

Mheshimiwa Sumaye alitoa shukurani kwa WaTanzania waliomsaidia akiwa masomoni. Alisema kuwa maisha yake chuoni Marekani yamekuwa tofauti na maisha aliyozoea Tanzania ya kuwa na wahudumu, walinzi, wapishi nk. Alisema alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na alikuwa anajipikia, kujifulia, kufanya usafi na kubeba backpack ya vitabu kwenda darasani. Pia alikuwa na homework kibao na mwanzo aliona ni kazi kweli lakini alizoea.

Alicheskesha watu alivyosema kuwa Tanzania alizoea kuitwa 'Mheshimiwa' lakini hapa USA hata mtoto mdogo anamwita, Fred.

Alitoa shukurani kwa waKenya pia waliomsaidia.

Sherehe kabambe iliandaliwa na waTanzania chuoni Harvard ya kumpongeza mhesimiwa Sumaye kwa kuhitimu masomo yake. Sherehe ilihudhuriwa na waKenya, waGanda, waGhana, na waNigeria, na wazungu kadhaa pia.

Mhesmiwa Sumaye anatarajia kurejea Tanzania hivi karibuni.