Thursday, June 07, 2007

Mheshimiwa Sumaye Atoa Shukrani kwa WaTanzania New England



Mheshimiwa Sumaye na mke wake Esther wakifungua densi.

Leo aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka kumi, mheshimwa Frederick Sumaye, amemaliza masomo yake na kuhutimu shahada ya juu ya Masters of Public Administration kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, John F. Kennedy School of Government mjini Cambridge, Massachusetts, USA.

Mheshimiwa Sumaye alitoa shukurani kwa WaTanzania waliomsaidia akiwa masomoni. Alisema kuwa maisha yake chuoni Marekani yamekuwa tofauti na maisha aliyozoea Tanzania ya kuwa na wahudumu, walinzi, wapishi nk. Alisema alikuwa mwanafunzi wa kawaida tu na alikuwa anajipikia, kujifulia, kufanya usafi na kubeba backpack ya vitabu kwenda darasani. Pia alikuwa na homework kibao na mwanzo aliona ni kazi kweli lakini alizoea.

Alicheskesha watu alivyosema kuwa Tanzania alizoea kuitwa 'Mheshimiwa' lakini hapa USA hata mtoto mdogo anamwita, Fred.

Alitoa shukurani kwa waKenya pia waliomsaidia.

Sherehe kabambe iliandaliwa na waTanzania chuoni Harvard ya kumpongeza mhesimiwa Sumaye kwa kuhitimu masomo yake. Sherehe ilihudhuriwa na waKenya, waGanda, waGhana, na waNigeria, na wazungu kadhaa pia.

Mhesmiwa Sumaye anatarajia kurejea Tanzania hivi karibuni.

30 comments:

Anonymous said...

him sailing on his ego trip talala talala,
blast him on his spaceship talala talala,
millions miles from reality, talala talala,
no care for you no care for me...

yangu macho tuu. BAE wameuza rada mazishi, kiasi kadhaa cha fweza kimerudi marekani.

Anonymous said...

Nampongeza sana mhe Sumaye kwa kujiendeleza.

Anonymous said...

Hongera "Fred" kwa kuhitimu masomo yako pale Harvard.

KakaTrio said...

whatever the reason for him to go back to school, I congratulate him fo r getting his Masters degree. Now go for Phd Fred and then go back to teach Tanzania kids you denied opoortunity to go to school for that is the only good thing you can do for them.

Anonymous said...

Hi Fred go back to Tanzania and preach to those kids how important education is... and if they get the chance they must use it!! Shule uzeeni sio tamu kwani yes utabakiwa na elimu tuu but umri umekwenda sio rahisi kuitumia ipasavyo.. probably in the next few years utatakiwa kustaafu.. what the worse.. si bora hiyo chance angeitumia kijana damu mbichi...

well hongera pia ni mfano wa kuigwa ni wachache sana especially wakifikia kwenye ngazi yako kimaisha wanakumbuka kuwa kuna umuhimu wa kujiendeleza... well done

Anonymous said...

Only in Africa, first u become a PM, then a student.

Anonymous said...

Huyu kilaza na mwizi mkubwa mwache adumbue alivyotuibia wakati ndugu zetu wanasota huko vijijini.

Eti waziri mkuu kwanza halafu ndipo ukasome; ukipunga kweli ule.

Anonymous said...

Naomba kujua amegraduate akiwa na GPA gani?

Anonymous said...

anony wa 7.40
mie nafikiri swala la GPA si muhimu-cha maana ni kuwa "Fred" amepitia hiyo "process" ya kubukua, kufanya homework na kukujadiliana maswala mbalimbali na wanafunzi wenzake.

Anonymous said...

Jamani niwastue tu msije mkampa sifa za bure. Pale Harvard sehemu yenye ulaini zaidi ni Kennedy School of Government Zero. Masters ambayo ni kozi nane tu zenye hadhi ya shahada ya kwanza, kwa mfano somo la micro-economics ambayo kwao ni basic tu. habari zinasema pamoja na kichwa chake kizito bado alipata "A". Hii ni shahada ya kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa watu kama yeye, haina kitu. Nenda kwenye google tafuta. Lakini someni hii: Sumaye, whose term as PM ended in 2005, has enrolled as a mid-career student in the Edward S. Mason Program at the Kennedy School of Government (KSG) for the 2006-2007 academic year, according to KSG media relations manager Doug Gavel.
Kisha nenda kwenye hii tovuti:
http://www.fas.harvard.edu/~cafrica/scholars.shtml

Salamu zao.

Anonymous said...

kusoma ni kusoma,kasoma nini, grade gani?whats this got to do with you lot,simple minds zenu zinawahaunt. sadly, i am afraid to say haka katabia ni legacy ya founding fathers wetu,tumekosa exposure as such tunavamia any triviality just to make our presence felt. one thing for sure the Tanzanian generation maturing now has been exposed, hence will do away with these tabias GOD help us

Anonymous said...

Huyu ni mmoja kati ya kundi la viongozi wezi wakubwa Afrika,wameiba pesa zote za kuendeleza vyuo,mahospitali ya Tanzania,Africa. Wakitaka kusoma/Kutibiwa wanakimbilia nje ya nchi zao. Angesoma Chuo kikuu cha Dar es salaam aone hali halisi.. Akina Babangida/Obasanjo wanasoma kwao Nigeria.. tena kwenye vyuo walivyoanzisha...

Anonymous said...

Nawaunga mkono wenzangu waliosema ukweli na walioachana na kasumba ya mheshimiwa ya bongo! huyu ni mwizi na mlafi mkubwa. Arudi bongo akatibiwe hopitali zisizo na vifaa adu dawa na aendeshe kwenye mashimo, na mengineyo mengi yanaumiza roho kusema. Haya ndio aliyoyajenga.

Anonymous said...

Huyu mtu yeye na Mkapa wameiibia nchi mali nyinyi, wana miradi ambayo hata kama wangetawala kwa miaka 100 bila kutumia hata senti moja ya mishahara yao, wasingeweza kuimudu miradi hiyo. Ingekuwa Irak mimi ningejitolea bomu la muhanga kwa ajili ya nchi yangu nikaondoa udhia kwa kizazi kijacho.

Anonymous said...

Wewe Chemi uache ushamba wa kuandika WaGhana, sijui WaKenya, ndio lugha ya wapi hiyo? Una tatizo la elimu wewe.

Anonymous said...

Hongera sana Mh.Sumaye.Hongera zangu si kwa sababu umepata shahada ya pili ya utawala, kubwa ni: 1.Kutoa fundisho kwa viongozi wa nchi kufanya kazi kutokana na elimu/professionalism na sio kubabaisha tu.Hata kama watu watakulaumu ktk uongozi wako kama ulifanya vibaya, mimi binafsi sintokulaumu kwa sababu umedhihirisha kabisa kuwa ktk kipindi chako chote cha uwaziri mkuu (miaka 10) hukua na elimu ya uongozi (leadership and management).Sasa umeona umuhimu huo, hilo ni findisho kwa JK kuteua watu kutokana na MERITOCRACY (kama ilivyo principle of beurocracy as proposed by Max Weber).

2.Fundisho la pili ni kwamba,uamizi wa kuanza masomo upya ni kutoa mwelekeo kwa viongozi wa nchi.Muelekeo upi hapo?Ili kupunguza suala zima la rushwa na ubadhilifu wa fedha, viongozi wa juu hususani wenye nyadhifa za kisiasa kuwa na elimu ya kutosha wasiteteleke nini watafanya mara baada ya kutoka madarakani.Wengi huingia ktk rushwa na ubadhilifu wa fedha za umma kuhofia hatma yao ya maisha mara baada ya kipindi chao madarakani kikiisha.Ila kama unaelimu ya kutosha utaweza kufanya kazi mbadala.Mfano, Hayati Mwl.Nyeyere aliweza kutuinga vitabu na kusuhulisha migogoro mingi mara baada ya kutoka madarakani.

3.Viongozi wetu nao wajijue kuwa ni binadamu kama sisi.Mh.Sumaye ktk shukrani zake amesema kuwa alikua anaitwa FRED na "washkaji" wa Marekani.Hii inawakumbusha kua viongozi wasijione minungu watu, kuna leo na kesho.Kwa nchi zilizoendelea kama USA, UK viongozi ni watu walio na "shared values with citizens".

4.Ushauri wangu sasa: Naomba Mh.Sumaye ukirudi hapa usijiingize ktk siasa tena.Naomba kwa manufaa ya nchi, ukizingatia sasa wewe ni mwanazuoni, mtaalam wa utawala, unaweza kuwa consultant mzuri kwa JK na CCM kwa ujumla.Ushauri wako utaisaidia CCM, hasa kujua kutenganisha kati ya STATE & CCM. Wengi wana CCM wanaunganisha vitu hivi viwili, state-party fussion.Mfano; Mh.Rais JK alipofanya ziara ktk jiji la Dar na wilaya zake, ziara ya kiserikali alipofika wilayani Temeke aligawa kadi za CCM kwa wanasiasa waliotoka upinzani kama vile Tambwe Hiza.Sasa kwa elimu uliyoipata,tunaomba urekebishe hili ndani ya CCM waweze ktutofautisha kati ya ziara za CCM na za kiserikali."Fussion" hii kwa mtu asiye na taaluma ya utawala na demokrasia inamlazimisha kuelekea upepo wa Rais ulipo hata kama alikua mpinzani.Huu ni ubakaji wa demokrasia.

UDSM STUDENT
POLITICAL SCIENCE
msauzi101@yahoo.com

Anonymous said...

Ni kweli nchi yetu Tanzania inaongozwaga na VILAZA kama Sumaye-No wonder maendeleo ni NDOTO kwa mwendo huu. Tunaongozwa na viongozi wezi na huyu ndiyo mfano halisi! Nasikitika tu kuwa unarudi Tanzania KUIBA zaidi na kujiongezea mashamba na mali huku walala hoi wanakufa na njaa. Kuweni na huruma enyi viongozi wezi TUMEWACHOKA!

Anonymous said...

Nampongeza Sumaye kwa kuongeza elimu. Ila kitendo alichofanya na mwenzake Mkapa cha kuiibia Tanzania mamilioni ya Shilingi hakina budi kukemewa na wapenda maendeleo wote barani Africa. Tatizo moja tulilonalo Africa na especially Tanzania ni tabia ya viongozi kulindana wanapoondoka madarakani. Sielewi kwa nini mheshimiwa Rais Kikwete hataki kukubali anapoambiwa madudu yaliyofanywa na viongozi waliopita na hata wengine amewagawia madaraka ya uwaziri kwenye serikali yake. Kwa mwendo huu Tanzania hatutafika mahali na suala la maendeleo litabaki kuwa ndoto. Nimefurahishwa sana na habari za kuwajibishwa mawaziri wawili wa Uganda kwa tuhuma za rushwa. Mfano huu ni wa kuigwa hapa Tanzania. Mungu ibaraki Africa, Mungu ibariki Tanzania.

Anonymous said...

Kweli kusoma ni kitu kizuri sana ila kusoma huku kwa Sumaye kwangu ni kitandawili. Kweli kwa umri wake na wadhifa wake ni nini tena alikuwa anataka kwenye hiyo elimu. Kwanza tujiulize serikali imetumia fedha kiasi gani kulipia hiyo shule yake. Sidhani kama alitoa hela mfukoni kwake kwani kulikuwa na minong'one mingi sana ya wingi wa fedha za kumsomesha huyo kiongozi mstaafu. Hivi wewe Sumaye, umesoma ili ukagombanie tena madaraka? Ulifanya nini kwa miaka yako kumi kama waziri mkuu? Unadhani hata upewe miaka mingine 20, utazidi kununua vijivi vya TZ kwa ajili yako binafsi au utawaletea wananchi wa TZ maendeleo haya wale wa Arusha? Kama bado unataka madara, unadhani hakuna watanzania wengine vijana wenye uwezo wa kuongoza kuliko wewe? Kwa kweli wakati mwingine tumuogope MUNGU. Hiyo hela uliosomea Sumaye ingekarabati shuel ngapi za msingi za TZ ache kujenga mpya vijiji?
MUNGU ibariki Afrika, MUNGU Tanzania.

Anonymous said...

Aliyezoe vya kunyonga vya kuchinja hawezi. Sasa hivi udenda unamtoka arudi akawanie NEC aandeleze wizi. Hahitaji hongera za yeyote.

Anonymous said...

Naona siyo vichekesho tu bali mzaha. Kila sifa nzuri wataka wawe nayo hata bila ubavu. Fredi hata shahada ya kwanza Mzumbe sidhani kama ana ubavu huo. Sasa hiyo masters ya miezi naona ni vichekesho tu. Labda nisome dissertation yake. Sidhani kama itakuwa hata na hadhi ya Special Project report. Wezi, waroho, wahujumu na wauwaji wakubwa wa uchumi wa taifa hawa. Kuitwa Fredi ndo tabu pekee aloiona shuleni? Mjinga mkubwa na sidhani kama ana nafasi ya kuelimika kabisa huyu.

MARK MAMBO said...

Well, What next ? Vying for the EA Presidency ?

Anonymous said...

Nyinyi watu inaelekea kuna kitu kinawasumbua, kwanza, kutokujua kwenu ni kwa kiwango kikubwa sana juu ya nchi yenu. Tanzania ya leo si ya jana. Kila kitu mnakiangalia kwa dharau tu, mnafikiri kukaa marekani ni sifa au umanamba? wenye upeo na uwezo wao wa maana hawawezi kufanya kazik ya babysitter, au kuiosha vyombo au kufagia barabara. Njooni kazi bongo za maana zipo, ila uwe na maganda ya kueleweka. Ila kama ulikwisha kujilipua zamani kwa kuchana pasi yako na kuukana uraia wako wee baki tu hasira siye Bongo twapete, twabadili kazi kila siku, twaendesha magari ya maana twajenga nyumba za maana, twala vema maisha ni mazuri, bidii yako tu. kama huna kisomo basi endeleeni kusafisha masufuria na hasira zitawaua.

Anonymous said...

Congrats ex-Mh. Sumaye. Natumai hutakuwa na siasa za hasira tena. Rudi home uungane na waTz wenzio rulizungushe kwa kusonga mbele hili gurudumu la maendeleo.

Anonymous said...

Siasa ni siasa! Nategemea Sumaye kajifunza mengi hasa pale aliposema "TZ naitwa mheshimiwa, lakini US hata mtoto aniita Fred". Ili TZ iendelee ni lazima viongozi watoe mawazo kuwa wao wateule au MIUNGU WADOGO. Waliojuu ya sheria ya TZ. Leo BLOG yote imejaa "ANONYMOUS" kwa sababu hakuna awezaye kuonyesha sura yake kwa MUNGU mtu. Thubutu utakiona!!

Sumaye arudi nyumbani kugombea nafasi ya "NEC" nia ni kujiandaa kwa nafasi ya urais 2015, mmm ndugu yangu kula imetosha ni bora ustaafu ktk siasa. Tunahitaji amani TZ, kuwepo KWAKO KTK UONGOZI ni hatari kwa amani ya TZ.

Mwishoni napenda kusema kuwa wtanzania tusikatswe tamaa na wachache wanaohuisha DEMOKRASIA TZ, tumeipigania hiyo toka pale Mwl Nyerere alipouwa vyama vingi na kubakiza TANU. Leo hii lengo limetimia, miaka 15 ya vyama vingi, pahala pa waTZ kusikika sauti zao pameongezeka, blog, radio, magazeti, tv n.k. HALUTA KONTINUA!!!!!!

Anonymous said...

HIVI JAMANI HAWATAKIWI KUWA WASOMI KWANZA NDIO WAWE MAWAZIRI, MAANA HII DILI SIIELEWI, ETI VIONGOZI WA SERIKALI HALAFU WANARUDI SHULENI, SISI WENYE BACHELORS NA MASTERS ZETU BADO HATUPATI NAFASI KAMA HIZO, UNBELIVABLE, PIA NASIKIA HIZI DEGREE ZAO ZA UWAZIRI NI ZA JINA TU, WANAENDA KWA MUDA FULANI MARA OOH! UNASIKIA WANA DEGREE, RIDICULOUS!!, HALAFU WAO NDIO WANAKUWA WAGENI RASMI KWENYE GRADUATION KIBAO, SHAME ON THEM, AM NOT PROUD OF THEM AT ALL CAUSE I KNOW WHAT'S BEHIND HIT!!!!!!!

Anonymous said...

HARVARD SIO MCHEZO NA SOI LELEMAMA.
SOMA CV ZA KUWEZA KU-JOIN PALE KWENYE TOVUTI YAO. BW SUMAYE KAPATA
CHETI MURUA-TUACHE YALIYOPITA TUJENGE TAIFA NA KUENDELEZA DUNIA HII UPANDE WA AFRICA. HATA WASEMAJI
WANAOLAUMU MAPUNGUFU KADHA FRED S. WATUTANGAZIE YA KWAO KAMA WANA UJASIRI HUO-VINGINEVYO WAKAE KIMYA.
NAO BILA SHAKA WAKIPATA MADARAKA JE
WATAFANYA NINI-BASI WATWAMBIE SASA.
UKIWA NDANI ya ruling-class mambo MAZITO HUMO-JE WAO WAKO NJE AU NDANI YA KUNDI HILO.

Anonymous said...

Tunakubaliana na hilo lakini cha msingi hapa ni kuwa Sumaye aachane na siasa kwa sasa na ikiwezekana ajikite kwenye kuelimisha vijana wa kitanzania kutokana na elimu aliyoipata. Tanzania bado tunahitaji academicians zaidi ikizingatiwa kuwa kiasi cha vijana wanaojiunga na elimu ya juu inazidi kupanda. Haina sababu ya yeye kujiingiza kwenye siasa wakati ameshakula vya kutosha na kama kuwaibia watanzania kishaiba mpaka vya kula vitukuu na vilembwe. Kujiingiza kwake kwenye siasa kutazidi kutia kichefuchefu tukikumbuka kashfa ambazo alizipata wakati wa uongozi wake na mkuu wake ambapo viongozi wa Tanzania walijilimbikizia mali kama miungu watu. Sumaye imetosha waachie watanzania wengine waendeleze siasa ya Tanzania.

Anonymous said...

Nampongeza Sumaye lakini angenifurahisha zaidi kama shahada hiyo angeisomea hapa nyumbani kwani tabu ipo wapi? si ni vyuo walivyovijengea misingi wenyewe wakati wa uongozi wao kwanini wanavikimbia.Nahisi shahada aliyoipata ni rahisi tu na kam angekuwa ndio anaombakazi leo serikalini asingapta kazi.Labda kwingineko

Anonymous said...

It is was a good retreat for Sumaye. And i congratulate him for decision he took. It showed he was realy prepared for life after politics. It gave him a good opportunity to see life from ground zero. BRAVO. Last but noy least. He has no good reason to hide, no enemies, he was just a simple politician, that is why he decided to go back to school as simple as any other mlala hoi hai.
Bravo, Sumaye. you did to Tanzanians what you could do best, i dont know anything bad that you did to us.