Showing posts with label Swine Flu. Show all posts
Showing posts with label Swine Flu. Show all posts

Thursday, October 01, 2009

Swine Flu (H1N1) Nchini Tanzania - Taarifa!


Taarifa Maalum Kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu hali ya ugonjwa wa Mafua Makali ya Nguruwe (Influenza A H1N1), Ikiwa ni taarifa ya tatu kutolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tangu ugonjwa huu uingie hapa nchini.

Ugonjwa huu kwa mara ya kwanza ulitokea katika nchi ya Mexico mwanzoni mwa mwezi wa Aprili 2009. Hadi hivi sasa nchi 24 katika bara la Afrika zimethibitisha kuwa na ugonjwa huo, zikiwa na jumla ya wagonjwa 8,187 na vifo 41.

Nchi inayoongoza kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa katika bara la Afrika ni Afrika ya Kusini ambayo ina jumla ya wagonjwa 7,606 na vifo 31. Hadi kufikia tarehe 30/09/2009 idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huu hapa nchini ni 170.
Kati ya wagonjwa hao 151 ni kutoka mkoa wa Dar es salaam, 15 kutoka Wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara, na 4 kutoka mkoa wa Mara. Wengi wa wagonjwa hao walikwishatibiwa na kupona na kwa sasa hivi wagonjwa waliolazwa ni 15 ambao wapo wilayani Mbulu.

Vile vile, kati ya wagonjwa hao 170, kuna Watanzania 80. Hii inaonyesha kwamba, maambukizi ya ugonjwa huu yameanza kuingia kwenye jamii yetu. Aidha, hali ya sasa ya ugonjwa inaonyesha kuwa maambukizi yametokea katika shule mbalimbali za mkoa wa Dar es salaam. Sababu kubwa ni kwamba, virusi vya ugonjwa huu huenea kwa haraka kwenye mikusanyiko ya watoto, kundi ambalo limethibitishwa kisayansi kuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Ugonjwa huo.

Idadi ya shule zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa huu mpaka sasa, zilizoko katika mkoa wa Dar es salaam ni 9. Shule hizo ni pamoja na International School of Tanganyika, Delhi Primary School, Little Scholar, French Primary School, Dar es salaam International School, Msasani Peninsular Primary School, Feza Girls Secondary School, Makongo Secondary school na Litlle Deau Mont.

Wagonjwa wengi waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huu hapa nchini hawakuwa na dalili kali za ugonjwa huo, na walipona kati ya siku 3 hadi 5 baada ya kupatiwa matibabu. Wizara imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na ugonjwa huo ambapo: ·

Imeimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa ugonjwa huu, katika viwanja vya ndege, mipakani pamoja na bandari.
· Imeimarisha Ufuatiliaji na Utambuzi wa ugonjwa huu katika hospitali za rufaa, mikoa na wilaya na kuunda kamati za wataalamu za kitaifa, mikoa na wilaya ili kupambana na ugonjwa huu

· Pia mafunzo yametolewa kwa watumishi wa afya katika hospitali za rufaa, mikoa pamoja na kamati za afya za wilaya kuhusiana na ugonjwa huu.

· Wizara imepeleka vifaa kinga katika hospitali zote za rufaa na mikoa pamoja na dawa (Tamiflu) dozi 1000 kwenye hospitali zote za rufaa, mikoa na wilaya.

· Wizara ilitembelea na kufanya majadiliano na uongozi wa hospitali binafsi za mkoa wa Dar es salaam, na imezipatia mafunzo pamoja na dawa za ugonjwa huu.

· Huduma za upimaji pamoja na dawa zinatolewa bila malipo.

· Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa mganga mkuu wa jiji la Dar es salaam pamoja na manispaa zake imeimarisha ufuatiliaji katika shule zote zilizoathirika na ugonjwa huu, ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huu mashuleni.

· Wizara imesambaza vipeperushi na imeendelea kutoa elimu ya afya kuhusu ugonjwa huo kupitia njia mbalimbali za mawasiliano kama vile televisheni, radio pamoja na magazeti.

TAHADHARI
Wizara inapenda kuufahamisha Umma kuwa, ugonjwa huu hauambukizwi kwa kula nyama ya nguruwe. Njia kuu ya maambukizi ni kwa njia ya hewa iwapo mgonjwa atakohoa au kupiga chafya bila kufunika pua au mdomo, au kwa kugusa sehemu zenye virusi hivyo na kujigusa mdomomi au puani.


HITIMISHO
Kwa kuzingatia hali hiyo, Wizara inapenda kuwaelekeza wananchi KUNAWA MIKONO VIZURI KWA SABUNI NA MAJI MARA KWA MARA na pia KUZUIA MDOMO NA PUA KWA KITAMBAA AU KARATASI LAINI (TISSUE PAPER) WAKATI WA KUKOHOA AU KUPIGA CHAFYA. Pia, wananchi wanashauriwa kutoa taarifa haraka kwenye kituo chochote cha matibabu, mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.

Blandina S. J. Nyoni
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Thursday, July 09, 2009

Swine Flu Umefika Bongo... Mzungu Kauleta!

Duh! Kuna habari kuwa kijana wa kizungu kutoka Uiingereza anaumwa Swine Flu (homa ya nguruwe) huko Muhimbili. Inaelekea atapona, lakini sijui atakuwa ameusambaza kwa watu wangapi kabla hajatibiwa. Na huo ugonjwa ni wa ajabu, wengine wanaugua kidogo, wengine hoi na wengine wanakufa! Mungu atunusuru.

**************************************************************************
First A/H1N1 flu case confirmed in Tanzania

2009-07-09

DAR ES SALAAM, July 9 (Xinhua) -- The first A/H1N1 flu case confirmed in Tanzania was a British student who was hospitalized earlier this month, Tanzanian medical official told Xinhua on Thursday.

The male teenager was among a group of students and teachers who flew into the east African country from Britain via Kenya several days ago to carry out volunteer work, Andrew Swai, director of clinical services at the country's main referral hospital Muhimbili National Hospital, said to Xinhua on phone.

"He is well now, not infectious, and will be out of hospital tomorrow," Swai noted, adding that earlier diagnostic test showed the victim was positive for A/H1N1.

Preparations for the epidemic have already started in Tanzania, while the Ministry for Livestock Development and Fisheries is working closely with health, tourism, home affairs and infrastructure ministries to monitor the flu, according to government officials.

Before Tanzania, Kenya, Uganda and Ethiopia in east Africa had already confirmed their first A/H1N1 cases in recent days.

So far, A/H1N1 flu has infected more than 94,000 people in the world, including 429 deaths, according to the World Health Organization.

*************************************

Arusha, Tanzania - Tanzania's deputy minister of health says a visiting British student has been confirmed as the country's first case of swine flu.

The east African nation is the fourth African country to report a confirmed case of the H1N1 virus.

Deputy Minister Dr Aisha Kigoda said Thursday the student arrived in the commercial capital of Dar es Salaam a week ago as part of a group of volunteer students. The student told immigration officials he felt unwell and was sent to hospital immediately.

Kigoda says Tanzania has contingency plans in place to contain the virus.

The World Health Organisation has confirmed 429 deaths from the virus worldwide and nearly 95 000 infections since it was first reported in Mexico in March. - Sapa-AP

Tuesday, April 28, 2009

Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe (Swine Flu)


Duh! Wadau, hapa Marekani watu wana haha ile mbaya kwa hofu ya kuambukizwa ugonjwa wa SWINE FLU! Mwaka juzi ilikuwa homa ya ndege (bird flu), mwaka huu ni homa ya nguruwe.

Nakuambia, mtu akikohoa, akipiga chafya, watu wanamtazama mara ishirini! Wanopanda kwenye suubway na masabi kwenda kazini wana wasiwasi kuwa wataambukizwa. Huko makazini, waliosafiri kwenda Mexico wanaambiwa wakae nyumbani mpaka walete vyeti kusema kuwa ni wazima wa afya. Wataalamu wanasema kuwa kiini (epicenter) cha huo ugonjwa ni Mexico.
Huko Scotland kuna mke na mume waliofunga ndoa hivo karibuni na walikuwa kwenye Honeymoon huko Mexico. Leo kuna habari kuwa wote wawili ni wagonjwa. Doh! Waliosafiri nao kwenye ndege ni wazima kweli?
Huo ugonjwa unaambukizwa kirahisi, hivyo mtu moja akiingia kwenye jengo, mamaia ya watu wanaweza kuumwa. Na huko Mexico maelefu ya watu wanaumwa na mamia wamekufa! Wataalamu wanasema huo ni mwanzo maelfu na maelfu ya watu wataaugua na kufa.

Mungu atunusuru kwa kweli. Kwa sasa bado hatujasikia kesi ya mtu hapa Massachusetts, lakini watu wavayo safiri safiri kwa gari, ndege, treni, lazime ugonjwa utaingia punde tu.


****************************************************

ATLANTA – The number of confirmed swine flu cases in the United States has jumped to 64, federal officials said Tuesday, and states reported at least four more.

The U.S. Centers for Disease Control and Prevention said the new count includes "a number of hospitalizations." CDC officials had previously said just one person had been hospitalized.
The CDC said there were 17 new cases in New York City, four more in Texas and three additional cases in California. That brings the total numbers of cases confirmed by federal officials to 45 in New York City, 10 in California, six in Texas, two in Kansas and one in Ohio.
State health officials in California have confirmed three other cases, and Indiana authorities have confirmed one.

The increase is not surprising. For days, CDC officials have said they expected to see more confirmed cases — and more severe illnesses. Health officials across the country have stepped up efforts to look for cases, especially among people with flu-like illness who had traveled to Mexico.
CDC officials also warned that updates in the number of confirmed cases would at time be disjointed, as different states announce new information before the CDC's national count is updated.