Wadau katika Sinema That's My Boy, ambayo imetoka kwenye theaters wiki hii, mimi nilikuwa Stand In wa Luenell ambaye anaigiza katika hii sinema kama Champale ambaye ni Stripper (mvuo nguo). Champale ni mama mtu mzima anayepnda kutembea na matiti nje. Matiti ambayo mnaona ni feki. Kazi ya Stand In ni kuhakikisha kuwa mwanga, microphone nk. ziko sawa kabla ya Stelingi kuingia kufanya kazi yake. Kila kitu ambayo utaona kafanya Luenell, nilifanya mimi kwanza. Wali-shoot mwaka jana katka sehemu mbalimbali Massachusetts.
Katika kideo hii walikuwa wananitumia kupima rigging kwenye pole kwa vile mimi na Luenell tulikuwa na uzito sawa. Nilifundishwa siku kadhaa kabla ya hayo mazoezi jinsi ya kupanda hiyo pole. Hivyo alipoingia kufanya kazi yake ilienda smooth. Hii ni ile scene ambayo anakul mayai na sausage. Nilishinda nao wiki nzima katika seti ya Strip Club. Ni wiki ambayo sitasahau maishani mwangu. Kama unatafuta sinema ya kuangali wiki hii napendekeza That' s My Boy!
Kwa vile sinema imetoka narushusiwa kuongea kuhusu ushirikiano wango katika hiyo sinema. Lazima niseme kuwa Adam Sandler ni mtu poa sana.
![]() |
| Picha kutoka Sinema, niliinginiwa sana kichwa chini miguu juu kabla ya Luenell kuingia kufanya kazi yake. |
| Mimi na Lunell mwaka jana kwenye set ya That's My Boy. Hayo matiti ni feki! You can Read a Review of That's My Boy HERE: |




