Showing posts with label Vitenge. Show all posts
Showing posts with label Vitenge. Show all posts

Monday, July 01, 2013

Ziara ya Rais Obama wa Marekani Nchini Tanzania Katika Picha

Wadau,  vyombo vya habari hapa Marekani jinsi waTanzania walivyompokea Rais Obama kwa upendo na ukarimu.  Na pia walishanaa Rais Bush Jr. alivyopokelewa. Kweli waTanzania tujivunie! Wanazidi kushangaa vitenge na khanga zenye picha ya Rais Obama pia! 

Picha Kutoka Yahoo News na CNN.com






Thursday, November 04, 2010

Makochi ya Vitenge




Mwaka 1990 kuna dada fulani (Marehemu) huko Manzese aliyetengeneza maforonya na mashuka ya vitenge. Watu walimcheka.

Leo wazungu wanatengeneza makochi ambayo yamefunikwa (upholstery) na vitenge. Tena wanaziuza bei mbaya. Hebu cheki hizo kochi pichani, moja dola $1,700! Hizo ottoman za kuwekea miguu dola $200! Acheni kudharua vitenge na khanga zetu. Tengenezeni maseti ya mashuka na maforonya mpate kibunda....ohhooooo! Exported from Tanzania!
Mnaweza kuona bidhaa zaidi kwa kubfoya hapa: ANTHROPOLGIE.COM