Mungu nisamehe! Leo nimecheka kweli nilivyosikia kuwa saa aina ya Rolex, ya O.J. Simpson ni feki. Ina thamani ya dola $100 tu na siyo $40,000. Kumbe ni feki na ilitengenezwa China.
Sasa sijui huyo Fred Goldman, baba yake marehemu Ron Goldman aliyeuliwa pamoja na mke wa OJ. Nicole Brown Simpson mwaka 1994 anasemaje. Huyo Fred Goldman anataka kumnyang'anya OJ kila kitu chake cha thamani. Alivyona O.J. kavaa hiyo saa kwenye show ya TMZ, alitoa amri kwa wanasheria wake waichukue na wauze.
Kesi ilienda mahakamani na O.J. alikubali kutoa hiyo saa bila kupinga. Alisema saa enyewe alinunua kwa dola $125 na siyo $40,000 kama alivyodai Fred Goldman. Wanasheria waliipeleka kwa wataalam kuitathmini. Walisema thamani yake ni dola $100 tu.
Sasa mahakama wamemwambia Fred Goldman na wanasheria wake kuwa lazima hiyo saa irudishwe kwa O.J. japo walisema wana mtu ambaye alikuwa tayari kuinunua kwa dola $20,00 kwa vile ni mali ya OJ. Mahakama ilikataa kwa vile walisema wakichukua kitu kisicho na thamani kubwa basi watakuwa na uchu na kutaka kuchukua vitu vidogo vidogo mpaka chupi na itakuwa balaa.
Kabla ya hiyo kesi O.J. alikuwa anapendwa kwa vile alikuwa ni mcheza Football na mcheza sinema maarufu.
Sasa watu wanauliza, Fred Goldman akipata hizo pesa na vitu vya thamani, mtoto wake Ron ata fufuka? Pia wanauliza kwa nini anadai kuumizwa kupindukia na kifo cha huyo mtoto wake alikuja hajaongea wala kumwona mtoto wake miaka kabla ya kifo chake? Ron Goldman alipata matatizo na huyo baba yake Fred alikataa kumsaidia akiwa hai. Sasa watu wamempachika Fred Goldman, jina Fred Goldiggerman. Ni kweli kuna uchungu kumpoteza mtoto lakini matendo yake kutafuta pesa sasa zinampa Fred Goldmna jina baya.
Kwa wasiojua OJ aliachiwa huru na mahakama katika kesi ya mauji ya Ron Goldman na Denise Brown Simpson. Weusi waliona kuwa OJ hana hatia na wazungu waliona ana hatia. Si ajabu maana Marekani maelefu na maelfu ya watu weusi waliuliwa na wazungu na hakuna aliyepelekwa mahakamani wala kushitakiwa. Inatokana na historia ya Utumwa na ubgauzi hapa Marekani. baada ya Oj kuachiwa huru alienda kwenye mahakama ya Civil, na kupewa judgement dhidi ya OJ ya dola 33 milioni. Lakini bado hajapata hizo pesa kutoka kwa OJ.
Hivi karibuni O.J. aliandika kitabu kuhusu jinsi angewaua Ron Goldman na mke wake. Ilikuwa initwa "If I did it!' (Kama nilifanya). Fred Goldman alienda mahakamni na kudai apewe hicho kitabu na haki zake zote, kapewa. Kabadilisha jina la kitabu na kuita, 'I did it' (Nimefanya)
Lakini watu hawakufurahi alivyofanya na hiyo kitabu. Wanasema kuwa kuitoa na kupata pesa na kuishi maisha ya kifahari nazyo ni kuishi kwa pesa zilizopakwa damu (blood money). Dada wa Nicole Brown na familia yake walimwita akina Goldman wanafiki. Oprah alimwuliza Fred Goldman kama haoni haya na matendo yake. Watu wanasema atafufute kazi siyo kuishi kwa pesa za OJ kama anavyofanya.
Haya tutaendelea kusika habari za Fred Goldiggerman na binti yake Kim.
Kwa habari zaidi za hiyo tukio someni:
http://ap.google.com/article/ALeqM5gwXXBU9-InHgXXvu-dN7FNTkDe_gD8S3C92G0
http://www.msnbc.msn.com/id/20759477/
http://boards.courttv.com/showthread.php?threadid=312130
http://www.foxnews.com/story/0,2933,212338,00.html
http://ap.google.com/article/ALeqM5gwXXBU9-InHgXXvu-dN7FNTkDe_gD8S1EQ380





