Saturday, October 06, 2007

Fred Goldman agonga Ukuta! Saa ya OJ aina ya Rolex ni Feki!

Picha iliyomtia kiwewe Fred Goldman

Fred Goldman na binti yake Kim



Mungu nisamehe! Leo nimecheka kweli nilivyosikia kuwa saa aina ya Rolex, ya O.J. Simpson ni feki. Ina thamani ya dola $100 tu na siyo $40,000. Kumbe ni feki na ilitengenezwa China.

Sasa sijui huyo Fred Goldman, baba yake marehemu Ron Goldman aliyeuliwa pamoja na mke wa OJ. Nicole Brown Simpson mwaka 1994 anasemaje. Huyo Fred Goldman anataka kumnyang'anya OJ kila kitu chake cha thamani. Alivyona O.J. kavaa hiyo saa kwenye show ya TMZ, alitoa amri kwa wanasheria wake waichukue na wauze.

Kesi ilienda mahakamani na O.J. alikubali kutoa hiyo saa bila kupinga. Alisema saa enyewe alinunua kwa dola $125 na siyo $40,000 kama alivyodai Fred Goldman. Wanasheria waliipeleka kwa wataalam kuitathmini. Walisema thamani yake ni dola $100 tu.

Sasa mahakama wamemwambia Fred Goldman na wanasheria wake kuwa lazima hiyo saa irudishwe kwa O.J. japo walisema wana mtu ambaye alikuwa tayari kuinunua kwa dola $20,00 kwa vile ni mali ya OJ. Mahakama ilikataa kwa vile walisema wakichukua kitu kisicho na thamani kubwa basi watakuwa na uchu na kutaka kuchukua vitu vidogo vidogo mpaka chupi na itakuwa balaa.

Kabla ya hiyo kesi O.J. alikuwa anapendwa kwa vile alikuwa ni mcheza Football na mcheza sinema maarufu.

Sasa watu wanauliza, Fred Goldman akipata hizo pesa na vitu vya thamani, mtoto wake Ron ata fufuka? Pia wanauliza kwa nini anadai kuumizwa kupindukia na kifo cha huyo mtoto wake alikuja hajaongea wala kumwona mtoto wake miaka kabla ya kifo chake? Ron Goldman alipata matatizo na huyo baba yake Fred alikataa kumsaidia akiwa hai. Sasa watu wamempachika Fred Goldman, jina Fred Goldiggerman. Ni kweli kuna uchungu kumpoteza mtoto lakini matendo yake kutafuta pesa sasa zinampa Fred Goldmna jina baya.

Kwa wasiojua OJ aliachiwa huru na mahakama katika kesi ya mauji ya Ron Goldman na Denise Brown Simpson. Weusi waliona kuwa OJ hana hatia na wazungu waliona ana hatia. Si ajabu maana Marekani maelefu na maelfu ya watu weusi waliuliwa na wazungu na hakuna aliyepelekwa mahakamani wala kushitakiwa. Inatokana na historia ya Utumwa na ubgauzi hapa Marekani. baada ya Oj kuachiwa huru alienda kwenye mahakama ya Civil, na kupewa judgement dhidi ya OJ ya dola 33 milioni. Lakini bado hajapata hizo pesa kutoka kwa OJ.

Hivi karibuni O.J. aliandika kitabu kuhusu jinsi angewaua Ron Goldman na mke wake. Ilikuwa initwa "If I did it!' (Kama nilifanya). Fred Goldman alienda mahakamni na kudai apewe hicho kitabu na haki zake zote, kapewa. Kabadilisha jina la kitabu na kuita, 'I did it' (Nimefanya)

Lakini watu hawakufurahi alivyofanya na hiyo kitabu. Wanasema kuwa kuitoa na kupata pesa na kuishi maisha ya kifahari nazyo ni kuishi kwa pesa zilizopakwa damu (blood money). Dada wa Nicole Brown na familia yake walimwita akina Goldman wanafiki. Oprah alimwuliza Fred Goldman kama haoni haya na matendo yake. Watu wanasema atafufute kazi siyo kuishi kwa pesa za OJ kama anavyofanya.

Haya tutaendelea kusika habari za Fred Goldiggerman na binti yake Kim.

Kwa habari zaidi za hiyo tukio someni:

http://ap.google.com/article/ALeqM5gwXXBU9-InHgXXvu-dN7FNTkDe_gD8S3C92G0

http://www.msnbc.msn.com/id/20759477/

http://boards.courttv.com/showthread.php?threadid=312130

http://www.foxnews.com/story/0,2933,212338,00.html

http://ap.google.com/article/ALeqM5gwXXBU9-InHgXXvu-dN7FNTkDe_gD8S1EQ380

8 comments:

Anonymous said...

hello chemi!
nakumbuka ulitoa habari za coorey david anaomba watu wa kuchat nao akiwa jela,now ametoka hata kusema asante ameshindwa?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 5:56am,

Nitamtafuta halafu nitatoa update.

Anonymous said...

wewe chemi unaonekana ni pro OJ, this man is just lucky to be free,kwa sababu ni mmatumbi mwenzio unapoteza rational reasoning

Anonymous said...

hivi chemi huyu mzee ana haki ya kuchukua kila kitu cha OJ? mbona anamnya nyasa sana mzee OJ.
Au sijaelewa unaweza kunifafanulia hapo iweje achukue kila cha oJ cha thamani na wakati OJ alishinda kesi?. na $mil 33 aliambiwa kulipwa kwa madhumuni gani?

Anonymous said...

Na bado watu tutasikia O.J. ni TEFLON O.J. hizo charges za Las Veags zitaishia hivi hivi. O.J. amachanjwa!

Anonymous said...

There is no question that Mr. Simpson is a very lucky man. He can attribute that to his African roots. Has he done the DNA testing? Does he know his African roots?

Anonymous said...

mimi binafsi nasema wazi namsupport oj why? kwa sababu hana kosa hamna alichofanya .kama ni kuua hajaua mtu labda ninyi wenzangu mana ushahidi kwamba alimwua mkewena na boyfriend wa mkewe basi mniambie

pili kwa kuwa ni mtu mweusi namsupporty no matter what huku marekani suala liko wazi issue ya oj ni issue ya rangi ya ngozi na wazungu wanataka afe! period!

lakini cha kujiuliza hapa ni kwamba kama huyu oj angelikuwa mzungu na mahakama ilisema hajaua mtu hivi manfikri media na wazungu wenyewe wangewaruhu watu kujadili hili suala tena kujudge na kumhukumu kiasi hicho?

wao wazungu wameua wangapi weusi kwa kuwa lynch miaka hiyoo tena bila hata mtu kupelekwa mahakamani au kufunguliwa mashitaka na kesi kuendeshwa walipewa right ya kuchinja au kuua mnyama huyu mweusi saa na wakati wanaopenda .lakini hilo hawalioni!

pia kesi ya oj siyo ya kuuua mtu ni juu ya kwenda kuchukua mali zake pale hotelini
waafrika tulio huku tusiwe wanafiki manjua fika na kweli kabisa sisi huku ni chini ya mbwa wa mzungu yaani mbwa na hata bugsa huku wana haki sana kuliko binadamu mweusi
HUMANE SOCIETY wanamtetea myama kuliko binadamu mweusi why?

huko canada mwaka 2006 black mmoja kijana alipigwa risasi 9 na officers wawili .uliza sababu sasa,eti alionyesha dalili za kutaka kum-stab mbwa wa polisi
kesi iliunguruma na ikazimwa hivi sasa maofisa wanendele kula donati na wancruise streets kama vile nothing has happened

OJ brother you are not perfect ,and so am i and so is everyliving creature
you are suffering for nothing but your skin color period!

Anonymous said...

More POWER to O.J.! Shame on Fred the Goldigger Goldman. The Brown's have a charity assisting victims of Domestic Violence. They have distanced themselves from the greedy hypocrite Goldiggerman.

Get a Life Mr. Goldman! Your son won't come back from the dead. Plus your actions make you look greedy.

Let's remember O.J. was judged to be innocent so why does every white person in America think he is guilty.