Saturday, August 20, 2016

Mashindano ya Miss Mwanza 2016

Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016, kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza walijitosa kusaka taji hilo.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo, Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.

Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment" na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE 2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016 waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano hilo.
Na BMG
Miss Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza 2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016.
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Majaji walikuwa na Kazi pevu kuchagua mshindi
Baadhi ya waliohudhuria kwenye tukio
Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akidondosha burudani kwenye Miss Mwanza 2016
Burudani za kiafrika pia zilikuwepo
Mkali wa Moyo Mashine, Ben Pol, alidondosha burudani poa sana
Ben Pol kazini
Kupitia BMG, Ben Pol, aliwashukuru wakazi wa Jiji la Mwanza kwa namna wanavyopenda kazi zake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi.
Miss Mwanza 2016 aliiambia BMG kwamba, maandalizi yake mazuri ndiyo yaliyompa fursa ya kunyakua taji hilo na kwamba amejiandaa vyema kwa ajili ya taji la Miss Lake Zone 2016 na pia Miss Tanzania 2016.
Miss Mwanza 2016 nambari mbili akibonga na BMG. Anasema shauku yake ni kuongeza juhudi zaidi ili kunyakua taji la Miss Lake Zone 2016.

Friday, August 19, 2016

Benki ya Dunia Kuendelea Kusaidia Sekta ya Maji Nchini

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua  kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam.
KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO). 

Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi. 

Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.

“Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji” alisema Bi. Bird

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.

“Changamoto ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo” alisema Mhandisi Luhemeja.

Benki ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo, pamoja na Uchumi na Biashara.


Sunday, August 14, 2016

Tanzia - Mh. Mzee Aboud Jumbe

Rest in peace Mh. Mzee Aboud Jumbe. (1920 - 2016)

Saturday, August 13, 2016

Paka Kichaa au Mjanja?


Huyo paka ni mjanja au kichaa? Anakubali kunyonyesha panya ambao ni chakula kikuu cha paka. Au anawanyonyesha ili wanone apate mlo safi?

Mwenyekiti Mpya wa CCM Dr. John Pombe Magufuli Apokelewa kwa Nderemo na Vifijo

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi waliofika Uwanjani hapo kumlaki leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndehe wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanaCCM pindi alipowasili Ofisi Ndogo ya Chama hicho, Mchana wa leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndg. Rajab Luhwavi mara baada ya kuwasili Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisaini Kitabu cha wageni kwenye Ofisi Ndogo ya CCM, iliopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikifanya Mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhan Madabiba.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana .
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwasalimia wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteja jambo na Wakuu wa Wilaya za Ilala (Sophia Mjema) na Kindondoni (Ally Hapi).



Tanzania Kutumia Dola Mil 500 Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchini

TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba  akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.


 Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi  kushoto ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi
TANZANIA inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza  juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.

“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.

Ambapo alisema katika kushiriki  juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .

Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa nchini.

“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani  Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.

Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Monday, August 01, 2016

Maandalizi ya Chakula Kutoka Mazingara Machafu!

Mnaopenda Kula restaurants, na chakula cha caterers..
halahala! Hizo kuku ziliingia kwenye michuzi, supu, roast, nk.  Halafu unashangaa Kwa nini tumbo inauma na unaharisha kesho yake.