Tuesday, July 11, 2006

Minjemba walikoma Boston!

Ninacheka! Na bado nacheka! Loh! Nimeanguka kwenye kiti, niko kwenye sakafu! Bado nacheka! Mbavu zinauma Jamani, nisaidie! Uwwwwiiiii!

Ni hivi, juzi nilienda kwenye klabu fulani Downtown Boston na rafiki yangu (dada Mmarekani mweusi). Ni msanii mwenzangu na tuliamua kufanya ‘Girls Night Out!” Tulikaa mezani na vinywaji vyetu na sahani ya buffalo wings (mabawa ya kuku enye pilipili). Karibu na sisi kulikuwa na wanaume wawili kutoka Tanzania tena ndo siku yao ya tatu hapa Marekani. Mimi siwajui na wao hawakunijua. Walikuwa wanaongea Kiswahili. Mimi nilijikausha tu, sikutaka wajue naelewa wanasema nini. Nikamwambia rafiki yangu kuwa hao wanaume ni wageni kutoka Tanzania. Aliniomba nimwintroduce kwao na mimi nakakubali ila baadaye kidogo.

Basi, hao minjemba, walikuwa wanasuka mipango ya kuopoa mademu wa kizungu hapo klabuni. Na kutokana na walivyokuwa wanaongea lazima walisuka mpango wa kuonja wazungu kutokea Bongo. Walikuwa wanamcheki kila dada hapo klabuni, mara huyo mbaya, yule mbaya, yule mwembamba, yule hana matako, matiti madogo, yule mzuri kidogo, huyo vile. Wakawa wanajadili watupe offa au la (hatukupata), lakini mmoja kasema nia yao ni kutoka hapo na wazungu. Wakawa wanacheki nani yuko na nani, na wakajadili jinsi ya kuwatongoza. Nikamwambia rafiki yangu walikuwa wanasema nini, tukawa tunacheka.

Basi, kwenye meza karibu na mimi kulikuwa na akina dada wawili wa kizungu, wazuri kweli kweli. Si kawaida yangu kusifia wazungu, lakini hao walikuwa ni wazuri, walijremba vizuri, walivaa vizuri, nywele ndefu zimechanwa vizuri mno, yaani ukiwaona unasema ni ‘perfect’. Tukasema lazima ni models. Walikuwa wamekaa wenyewe wanatazama mambo hapo klabuni. Naona hao minjemba ikawaona. Basi, walikunywa vinywaji vyao kusudi wapate moyo ya kuwa-approach.

Wimbo ukapigwa, na hakuna mzungu aliyewaomba densi, basi wale wakamka na kuwaomba densi. Wale akina dada, bila kusita walikubali. Ungeona nyuso za hao minjemba walivyokuwa na furaha. Wakacheza densi ya kwanza, wakacheza ya pili, mwisho wale akina dada walihamia kwenye meza ya hao minjemba.

Wakati huo watu klabuni wanawatazama, wengine walikuwa wanacheka. Na mimi nikawacheki vizuri. Nikasikiliza maongezi ya hao akina dada. Halafu nikacheki mikono yako, duh, mikubwa! Ikaniingia! DAH! Kumbe si akina dada hao ni midume! Ni ma transvestite! Sasa nikabakia nawatazama wa waBongo kwa mashangao! Nikasema hao akina kaka hawajui wameopoa akina nani, maana usoni walionekana kuwa na furaha kama vile wameshinda bahati nasibu! Na huyo rafiki yangu kaniambia tujiandae kwa ajili ya sinema ya bure.

Nilitaka kuondoka kuelekea kwenda nyumbani, lakini nikamua kukaa maana nilitaka kujua itaishia vipi. Wale akina kaka wakaanza kuwaambia, wako Boston kwenye business, na wako Hoteli fulani. Wakawa wanawaambia habari za Tanzania na kuwa ingekuwa vizuri siku moja wawatembelee huko. Wana majumba ya fahari, na watawapeleka mbuga za wanyama. Mwisho wakawakaribisha hotelini kwao kusudi wapate vinywaji zaidi. Pia walikuwa na zawadi kutoka Tanzania ambazo walitaka kuwapa. Nilishangaa, wale wawili wakasema, “Okaaay!” Basi wakaamka wakasema wanaenda restroom, kujipodoa halafu watarudi.

Walivyoinuka kwenda huko na mimi nikaona ni chensi ya kuwaonya. Rafiki yangu kaniambia nisiwaonye. Lakini nikasema bora niwaonye maana wakifika hoteli na wakikuta si wanawake inaweza kuwa balaa. Nikaamka na kwenda kwenye meza ya hao minjemba, nikawasalimia kwanza kizungu. “Hey guys, how are you?”

Wakajibu, “We are good” Nikasema kwa kiswahili, “Nafurahi kusikia hivyo!” Wakanitazama kwa mshangao, “Heh, Dada Mbongo wewe?”

Asante Pina Colada ulimi ukawa unateleza...nikajibu, “Mimi Mbongo ndiyo. Na nyie kama kaka zangu, nimeona niwaulize, mtawafanya, au mtafanywa?” Wale akina kaka wakajibu, “Heh, nini tena!’ Nikajua kuwa bado hawajajua wako na akina nani.

Nikawambia, “Hamjui kuwa hao akina dada wakizungu mliyonao ni akina kaka! Shauri zenu!” Ungeona nyuso zao, yaani ilikuwa “Kodak Moment!” Bahati mbaya camera niliacha nyumbani. Mmoja kaanza kuongea kwa kigugumizi, Yaa yaa nii, ni wa se se senge!” Nikajibu, “Naam!”

Ungeona ile minjemba ilivyoshikwa na wasiwasi. Mmoja kumwambia mwenzako, “We Bwana si nilikuambia wazuri mno hao na kwa nini wazungu wenzao hawakuwataka!” Waliinuka haraka, na mimi nilitia ndogo ndogo na kurudi mezani kwangu kwa rafiki yangu. Nikamweleza ilivyokuwa naye akawa anacheka kwa sauti mpaka watu klabuni wanatutazama. Rafiki yangu kasema wakome kutaka wazungu. Wale akina kaka wakatoka haraka, haraka klabuni kabla wale trans wamerudi kutoka restroom.

Wale trans wakarudi na kukuta minjemba wamekimbia! Walirudi kwenye ile meza yao ya awali. Wakaonekana na huzuni kidogo. Nikaona watu wengine wanacheka cheka nadhani walijua ilitokea nini. Na sisi tulitoka klabuni na ile minjemba sijui ilipotelea wapi! Naona walikodi teksi kwenda hotelini kwao.

Siku tatu zimepita, na mimi kila nikikumbuka nacheka. Jamani, hapa Marekani wakati mwingine huwezi kujua nani mwanaume, nani mwanamke. Wanawake wengine wanavaa kidume, wanatembea kidume, utadhani wanaume, na pia kuna wanaume kama hao wanapenda kuwa kama wanawake, tena ni wazuri kuliko wanawake.

Kwa hiyo, muangalie mnataka kuopoa nani. Najiuliza, je, wangefika huko hotelini sijui nani angekunjwa, maana na wale minjemba walikuwa wamekunywa hasa. Wangeenda huko hotelini na kukuta wako sawa nao, ingekuaje?!!

Mbavu sina jamani.

8 comments:

Kabinti said...

kwa kweli kisa hiki kimenichekesha sana! Asante kwa kuwaonya kwani wangepigwa na bumbuwazi wangepofika hotelini na kufanywa.

Mija Shija Sayi said...

Da Chemi nitarudi baadaye nikimaliza kucheka!!!

Chemi Che-Mponda said...

Mimi mwenyewe kila nikikumbuka nacheka. Hata kwenye subway nilianza kucheka mpaka watu wakadhania kichaa!

charahani said...

Haloo hii kweli inachekesha nakumbuka hata mimi pia niliwahi kusikia tukio la namna hii hapo hapo Marekani, lakini hilo lilikuwa tofauti kidogo la bwana mmoja wa Kimisri aliyekuwa katika mitaa ya Wasenge pale New York.
Si akawa anajikinga mvua kumbe hiyo mitaa ya kuanzia fifth avenue kule chini chini kuna mambo ya ajabu ajabu. Akajitokeza bwana mmoja akamuuliza are you a gay.
Yule Mmisri akakunja ngumi kutaka kupigana. Kumbe hakujua alipojikinga mvua ni mitaa maarufu ya wasenge.

ndesanjo said...

Hata kama huna mwanya ukimaliza kusoma hii lazima ucheke. Kucheka ni afya. Umetuongezea kama siku tatu hivi za kuishi!

Anonymous said...

serves them right for trying to buy aids!

John Mwaipopo said...

Chemi hii kali. Zikifululiza kama 10 hivi uhai wa mchekaji unaongezeka mara 10 hivi kama alivyosema Ndesanjo.

Charahani hebu kisimulie kisa hicho kiundani kwacho tucheke pia Ntakutembelea Tabata Relini siku moja.

fadhili said...

Mimi naiunga mkono mijemba hiyo maana imeonyesha urijali wao kwa wale ambao hawajafika boston huu ni mji mwenye vitongoji vya Mashoga hivyo nikiona kuna rijali wanatangatanga kumezea gauo basi hamna noma ni bora hivyo kuliko kumwona kaka yako wa kibongo akitwangwa mate na jibaba lenzie.