Thursday, July 20, 2006

Rais Bush Apata Ashki Mkutanoni!

Jamani, watu Marekani wamekuwa wakisema kuwa Rais Bush ana utaira fulani wa akili. Kama watu walikuwa hawaamini, nadhani sasa wanaamini.

Wiki hii Rais Bush yuko Urusi kwenye mkutano wa G-8 Summit, na marais na viongozi wa nchi kadhaa. Kiongozi pekee wa kike hapo ni waziri mkuu wa Ujerumani, Bi Angela Merkel. Basi Bush ailiingia kwenye ukumbi wa mkutano, sijui kaingiliwa na kitu gani, huyo anaanza kumpapasa mabega. Na yule mama kamfukuza haraka haraka! Kwa kweli hapa Marekani hiyo initwa unyanyasaji wa kijinsia (sexual harassment), na mtu anaweza kufukuzwa kazi kwa ajili hiyo. Je, Rais Clinton angefanya hivuo watu wangesema awe impeached (avuliwe urais)! Maana kaibisha taifa la Marekani.

Na kabla ya hiyo tukio ya kumpapasa alitukana alivyokuwa anaongea na Waziri Mkuu wa Uingereza, bwana Tony Blair. Alitamka neno 'shyt' akiongea kuhusu waarabu! Jamani kumsikia rais wa Marakeni akitukana ni maajabu na sijui kama imekwishawahi kutokea. Labda tuseme asante teknolojia dunia nzima inaweza kujua vituko vya Rais wa Marekani.

Watu wanasema ndo matokeo ya Bush kutokuwa na 'handlers' wake, akina Cheney, baba yake na Bi Condoleeza Rice. Na ndo matekeo ya kuongea bila scripts!

Ione clip hapa:
http://www.youtube.com/watch?v=q0tEQhaK4VM&search=bush%20back%20rub

6 comments:

Mija Shija Sayi said...

Niliposoma sikuamini vizuri nikaona nisakanye habari hii kwa undani zaidi, bahati nzuri nikabahatika kupata Video yake japo ni ya sekunde lakini imenifanya niamini.

Fungua hiyo chini halafu ubonyeze kwenye video mkono wa kushoto.

http://www.bild.t-online.de/BTO/news/aktuell/2006/07/18/merkel-bush-liebes-attacke/merkel-bush-liebes-attacke.html

Chemi Che-Mponda said...

Yaani aibu kweli! Hizo video ziko nyingi kwenye neti. Basi hao wachekeshaji kama Letterman, na Leno wanafurahi kweli. Nangojea skiti zao. Na wiki hii usikose Saturday Night Live na Mad TV.

Loh! Lakini jamani kweli ni kashfa kwa Urais Marekani.

Anonymous said...

Jamanii sijui nsema ni joto limemkolea kichwani au ndio ule eazimu wake umesha mpanda, si kutaka kumuabisha huyo mama wa watu..
au pengine anamzimia sasa hajapatia nafadsi ya kumtonya si unajuaapenzi yakizidi sometime the person can act as a fool.
lakini ni aibuuu wamarekani wakubali hilo

Anonymous said...

yaah i total agree with anonymous, bush trying to impress the lady...oooh gosh he pick the wrong time n place...poor him i think he needs 24/7 supervison before he do something vry serious....

Anonymous said...

Da chemi bwana kweli hiyo ilikuwa ashki kwani laura hakwenda nae.

Anonymous said...

Dada Chemi mzee mzima alichemsha kwani alishindwa kujizuia.Lakini yeye ni binadamu bwana kwa hiyo kama binadamu wengine ana mapungufu yake.Kwani kama anaweza kusema kuwa mahala fulani pana silaha za maangamizi halafu baadaye akasema hakuna si pengine alidhani huyo mama labda anaweza kuwa na silaha za maangamizi kaunta naona alikuwa hamuamini kwani naamini mzee mzima kwa sasa hawezi kuamini mtu yeyote yule inawezaka kila mtu kwake ni mhalifu hata kama ni mkubwa mwezie au kuna uhusiano wa karibu.Kwa hiyo jamani pengine alikuwa anatafuta silaha za maangamizi unajua tena watu siku hizi wamezidi kujtolea muhanga.HIVYO ILIBIDI AKACHEKI KAUNTA!