Friday, November 24, 2006

Niko Bongo!

Habari zenu wasomaji wapendwa. Niko Bongo Dar es Salaam. Nimetua juzi, kwa kweli ni joto sana lakini naona naanza kuzoea. Nimefurahi kufika nyumbani baada ya muda mrefu. Leo nimeenda mjini na kwa bahati nimegongana na watu wengi tu ambao nilikuwa nawafahamu. Naweza kuwa natembea halafu nasikia 'Che-Mponda!' Na cheki ni mtu nilimfahamu toka zamani.

Sasa jamani ile jengo la Daily News la zamani wanaifanyia nini? Naona Maktaba wamekarabati kwa nje. Maji ya kunywa ya chupa na phone cards ziko kila mahala, mawasiliano ni rahisi. Lakini barabara nyingi mbovu, na traffic jams ni mbaya! Yaani kutoka mjini kwenda Mbezi Beach ni two hours!

Nimepapenda Slipway! Ice Cream yako safi na ile Mashua Bar pale Beachfront safi sana. Halafu kuna ATM's kila mahala siku izi hakuna kwenda benki kusimama kwenye foleni ndefu. Nimshangaa kuona kuna hata Casino pale karibu na Greek Cub ya zamani karibu na Red Cross. Bongo kumeendelea hata hii internet nayo tumia ni nzuri sana na up to date!

Jamani nisiendelee maana umeme shida!

Mengine baadaye!

4 comments:

Anonymous said...

KARIBU SANA DA CHEMI NAIPENDA SANA SWAHILI TIME.I WISH NINGEKUONA IN PERSON UNIPE LIVE ZA USA!MA NAME IS CHRIS.

Anonymous said...

HARIBU BONGO..bora upate data ukawahadithie kina maliwaza na ms jaq

zeze

Anonymous said...

Chemi lakini acha mapozi we bado ni wafrica,eti bongo mbu,vumbi and all that,sikutegemea mtu kama wewe kusema hivyo.Sababu nasema hivyo ni kwamba you endured a lot to the point you are and this whole bongo thing will have seemed just like 3rd world and notin else

Chemi Che-Mponda said...

To anonymous wa 12:59am, Bongo kuna maendeleo sana. Si kama enzi za Mwalimu na mambo ya kadi ya kaya, mchele kwa magendo etc.! Supermarkets zimejaa vitu. Jamani mbona wazungu wengi sana huko siku hizi?

Nimetafunwa na mbu, even though nilikuwa napaka Mosquito repellent.