Thursday, November 30, 2006

Kila Mtu ana cell Phone Dar

Jamani, mawasiliano ya simu ni rahisi sana Dar. Cell phone nyingi, makampuni yanashindana kupata wateja, phone cards zinauzwa kila mahala, tena bei si mbaya hata shilingi 500/- unapata! Watu wengi wanazo! Mbona cell phone USA ni ghali sana, tena ukiweka kwenye credit kadi ndo unalaguliwa kabisa! USA wanaweza kujifunza kutoka Bongo!

Lakini jamani barabara mbovu sana Dar, tena sana! MAVUMBI!

Baadaye!

10 comments:

John Mwaipopo said...

Chemi mambo vipi.

Kwenye hili la barabara za vumbi you got it right lakini la kumiliki simu ama ndiyo ama hapana. hiyo mia tano kuipata kwake si kazi ndogo eti. Ni vile tu hatuna namna nyingine ya kuwasiliana. vinginevyo hata hiki cha kwangu ningekitupilia mbali.

Marekani si nasikia kuna mikataba ya mwezi hata dola 40, ambazo kwa hesabu ya zamani kidogo inaweza fikia shilingi zetu 50 elfu. Je ikiwa huyu jamaa anapata mathalani dola 1000 kwamwezi hiyo sio poa. Au vipi?

sijui tufanye nini, mwe!

Alamsiki

Unknown said...

cell phone zipo ila kwa kipato cha mtanzinia bado ni gharama sana .ndio maana tabia ya kubeep imeenea.bado kuna kitu kimoja nilikuwa nangoja ukione,ila nitakupa fununu.angalia tabia za watoa huduma.huduma ambayo una haki nayo mpaka uombe au umjue mtu.halafu angalia jinsi watoa huduma wanavyowafagilia "wazungu".airport mimi nilinyimwa kitrolley kwa sababu jamaa alikuwa anamkimbilia "mzungu"!!!mimi nilimuhurumia tu kwa sababu ni kutokujua tu...thats our beloved Tanzania,we have got to work on it!

Rama Msangi said...

Hii ndio Tanzania dadangu. ah!! Si ndio mnasema lakini kuwa uboreshwaji wa maisha uanzie vijijini na sio mijini? Tanzania sio kijijini kulinganisha na Marekani au kwingineko? Ila sasa uholela huo si ndio huo unawafanya maaskari kuzwa kila siku? mtu anapiga simu jamaa wanavunja huku, akimaliza anatupa chip ya 500, ananunua nyingine anasubiri askari wanaondoka yeye anafanya vitu vyake palepale walipokuwa. Mkifika mkimpigia hapatikani, ndio nitolee hiyo vijana wa mjini husema.

Karibu dar

Anonymous said...

Kutapakaa kwa simu ndio kunanifanya niamini kuwa hapo baadaye nyanya ya "moblogging," itakuwa na faida kubwa kwa nchi zinazoendelea. Yaani kublogu kwa kutumia simu za mkono (kutuma picha, kuandika, na hata kupodikasti (kuwa na aina ya redio ya mtandaoni).

Unajua ukiongelea Intaneti watu wengi husema, "aah, watu wenye kompyuta ni wachache." Watu hawa hawajui kuwa simu hizi za mkono ndio zinakuwa kompyuta siku hizi. Ushindani ukiendelea, bei zitaendelea kupungua, na mara utaona watu vijijini wanaanza kuwa na anuani za barua pepe na kusoma na kutuma barua pepe kutumia simu za mkono. Mara wanaanza kusoma blogu ya Chemi wakiwa wamepumzika baada ya kulima!

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni. Marcopolo nina story kali sana kutoa kuhusu hiyo habari ya kuhudumia wazungu vyema! Kwa sasa niko kwenye Kiosk London njiani kurudi Boston. Nitatoa habari zaidi!

Anonymous said...

Chemi kweli siku nyingi hujakanyaga bongo that`s why a little thing like cellphone scares you.Kuna wabongo kama wewe wanafikiri bongo ni like ze 60`s namshukuru mungu umepata makaratasi na nauli ya kuja bongo sio kila mtu anaweza kufanya hivyo,watu wengine lakini are just ignorant to the whole subject lakini wabongo wengine wanasingizia eti bongo is behind kwamba they can`t come over maana what if the get sick na hakuna proper healthcare,that is realy damnn isn`t dada Chemi?

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 1:09am, asante sana kwa mchango wako. No the cell phone issue did not scare me, I was actually impressed. In fact USA could learn from that system instead of the current one in which may people are overcharged and ripped off!

Kuhusu Healthcare, kuna maendeleo sana. Yale mambo ya kupanga foleni asubuhi hadi jioni hakuna tena kama unaenda Private! Actually I thought I had Malaria, nilenda Mt. Massana Hospital (private) wakanipima wakasema hamna! Very clean and professional as well! Niliwahi kukimbia Muhimbili miaka ya 90 shauri ya uchafu!

So yes, after a ten year absence it was nice to see all the progress! Ila jamani umeme, barabara nyingi mbovu na kuna vumbi sana!

Anonymous said...

Taratibu Chemi,
Nadhani Mwaipopo kaelezea vizuri sana kuhusu cell phone Bongo. Hakuna namna yeyote unaweza ukasema cell phone ni cheap Tanzania kuliko USA nasema no way. Ukiwashauri wa Marekani waige Tanzania labda unataka serikali iondoshwe madarakani kwani watu hawako tayari kurudi miaka 100 nyuma.
Tukokotoe kwa ufupi; Kadi ya sh. 5000 unapata chini ya dk 10. kwa dk hizo labda unaweza kupiga simu tatu kwa kujibana sana. Sasa kwa mantiki hiyo tuseme mtu ana simu tatu tu kwa siku maana yake ni 30 x 3 = 90. 90 x 5000 = 450,000! Ndio laki nne na hamsini elfu. Tupunguze iwe simu moja tu kwa siku maana hizo laki nne ni watz wachache mno wanaweza kumudu 30 x 1000 = 30000 kama dola 30 hivi.Maana yake hapo mtumiaji ana dakika tatu kwa siku. Marekani mtu anapata dak 600 hadi 1000 kwa hiyo hiyo dola 30.Tena kuna plan zingine night ni bure!! Ni nani ana nafuu hapa? Weye unaishi Marekani unajua watu wanavyotumia simu hata wakati mwingine hawana cha maana cha kuongea. Ni nani Tz anaweza kuwa kwenye simu saa nzima na mtu yule yule? Bado sana kwa Tanzania kudai cell phone ni rahisi labda kama Chemi ulikuwa unatumia cellullar ya mtu anayolipiwa kazini.
Ni kweli cellullar zimejaa lakini robo tatu zina ingiziwa dola mbili kila mwezi kuzuia zisifungwe au wenye mtandao wao wansema ku-keep account active.

Chemi Che-Mponda said...

makafoo,

Asante sana kwa maelezo yako. Umeeleza vizuri sana na umesema kweli. Nilikuwa natumia cell phone ya mama yangu na nilikuwa nawekea time. Na kweli kwa siku hata shs 10,000/ nilikuwa natumia. Hapa USA nina prepaid Verizon na mara nyingi situmii zaidi ya $20 kwa mwezi na napata bonus minutes kibao jioni na weekends.

Asante kwa mchango wako.

Unknown said...

Kama alivyosema makafoo, ingawa cell phones ni nyingi, ni ghali saaana. Kwa kiasi cha shs3 30,000 naweza kutumia cell phone yangu hapa Finland kwa mwezi mzima. Dar kiasi hicho ni matumizi ya siku tu!!