Sunday, November 26, 2006

Diary from Dar es Salaam

Haya, ni siku yangu ya tano Dar. Malalamiko yangu makuu ni:

Ukosefu wa umeme
Barabara mbovu
Maji shida
Mbu!

Nimetafunwa na mbu! Na nimetumia mosquito repellent. Labda wamekuwa sugu. Lakini wamekunywa damu ya Boston!

Niko Mbezi kwenye cafe iliyoko barabarani kabisa. Kwa kweli computer zao ni safi sana, kuliko cafe iliyoko karibu na nyumbani. Wale wana computer nzee na slow.

Vumbi na michanga!

Lakini jana nilikuwa kwenye sherehe ya arusi. Jamani kuna catering companies siku hizi! Juzi nilikuwa kwenye Graduation party, ilikuwa kama arusi Ama kweli Tanzania kumekuwa Party Culture!

9 comments:

Unknown said...

pole Chemi...ndio maisha ya nyumbani hayo na hayatabadilika kama sisi wenyewe hatutayabadilisha.Hiyo Cafe unayopo ya mbezi kama sikosei ni ile ya Imalaseko,mimi pia niliipenda hiyo cafe.

Chemi Che-Mponda said...

Cafe inaitwa Silver

Wewe bwana mavumbi, barabara mbovu lakini watu wakarimu!

Anonymous said...

Dada yangu umeshakua mzungu kiasi hicho,eti mchanga,mbu etc you couldn`t make a different btn a 3rd world and where you live at the moment.I feel bad for you ma friend.End the end of the day though you might end up there,so stop living you little bubling world.

Anonymous said...

Mbu, vumbi na traffic umezidi DAR!

Anonymous said...

Dada Che Mponda habari gani?
Pole sana na Karibu Nyumbani. Kama wahenga walivosema Nyumbani ni Nyumbani. katika matatizo uliyoyaorodhesha hapo Juu yote na Kuunga Mkono, lakini kilichonivuta vizuri kwenye PC hii ni Tatizo la mbu. Kuna sababu ambazo zinasababisha kuwepo na Mbu Bongo. Moja ya sababu hizo ni Mazingira yaliyoshene=i vichaka na Madimbwi(Hili ni la Msingi) lakini tusisahau Bongo ipo katika ukanda wa Kitropiki ambapo mbu ni sehemu ya Mazingira yake Murua. Tunashukluru mungu kusikia kwamba sasa hao wakubwa hasa huko unapokaa wamekubali na sisi kutumia kemikali za DDT kama wao ili mbu iwe ni hadithi na ajabu kama huko huko uishipo.

Semkae said...

Good diary.

kyekue said...

Dada,hayo ndio maisha ya hapa tanzania, shukuru mungu una mosquito repellant, una kwenda internet cafe na una fursa ya mambo mengi duniani usilalamike. Kuna watu wana shida dunia hii we acha tu. Nimejifunza...nina toa maoni kuhusu hali halisi za maisha yetu lakini silalamiki, ukiona kwako kuna...kwa mwenzako kunaungua ,nimesahau kidogo. Kuna watanzania wana shida huwezi amini

John Mwaipopo said...

Zemarcopolo what is you blog/website. I want to get to it.

Anonymous said...

Dada, nimeipenda hii blog yako. kuhusu mambo ya vumbi, mbu na umeme , hali hii aitabadilika mpaka tuchangua viongozi wapya na vijana maana ndio wanaopenda maendeleo ya kwa jumla, viongozi wetu wameongoza kwa miaka mingi wengine toka kabla sijazaliwa mpaka leo ni viongozi je tutategemea nini kutoka kwako..?