Thursday, December 14, 2006

Kariakoo = Carrier Corps

Hapo zamani za kale kabla ya magari, lori, petroli, basikeli, wazungu walitegemea binadamu na wanyama kubeba mizigo yao. Hao waafrika walioajiriwa waliona sifa kubwa kufanya kazi na mzungu na kulipwa.

Hao wabebaji wlaikuwa wanaitwa Carrier Corps, na baada ya 'kuswahililize' ndo ikawa jina la Kariakoo tunaoijua leo.

Kabla ya hao wa kulipwa waafrika walilazimshwa kubeba hiyo mizigo wakiwa kama watumwa. Historia ya mwafrika jamani.

Jamani cheki hiyo mizigo ilivyo mizito halafu fikiria unabeba kuanzia Dar hadi Mwanza, na wakati huo hakuna barabara. Lazima mizigo ilipotea, hasa kama mtu anaanguka nayo kutoka mlimani. Mtu unatembea nayo unatazama mbele huko nyoka anakuuma! Na, kama wabebabaji walikufa njiani nani alibeba mzigo wake?

Kama mmewahi kuona sinema za Tarzan na zingine zilizohusu Afrika, utaona mzungu alivyobebwa kwenye kiti na waafrika huko ana wabebabaji mizigo yake. Tena waafrika wakionekana wavivu wanachapwa kama punda! Ama kweli tumetoka mbali.

4 comments:

Anonymous said...

Chemi,
Hilo la nani anabeba mizigo baada ya kifo au suala kama hilo bila shaka katika safari kama hizo mizigo ilikuwa inapungua kadri walivyozidi kuchanja mbuga. Vitu vingi vilikuwa ni masurufu ya njiani hivyo kama waliondoka na mchele au unga au chochote walichokuwa wakila wakati huo vilikuwa vikipunguwa kadri walivyozidi kwenda mbele hadi walipofika kituo kingine nakuchukua masurufu kadri ya uwezo wao uliobakia

Mjengwa said...

Dada Chemi!
Hiyo picha hapo ni Kariakoo?
Asante sana kwa blogu nzuri yenye kuelimisha. Vipi, nilisoma umekuja bongo, je ulifika Iringa ama kupita?
Karibu sana!
/maggid

Baragumu said...

Chemi,Ni kweli mambo mengi ya zamani huwa yanasikitisha,lakini hata ukiangalia historia ya mataifa mengi na makabila yake pia yalipitia mambo mengi yenye mateso makubwa sana,yaani kwa wakati wao-walitamani vifo viwachukuwe,lakini Mwenyewe Mola ndie atakae wahukumu waliokuwa WENYE MABAVU na kuweza kuwatesa binadamu wenzao.

Anonymous said...

Chemi

Bado WaAfrika tunaendelea kuwa 'Carrier Corps' kwa namna nyingi: vita vya wenyewe kwa wenyewe; UKIMWI; madeni yasiyolipika; kudharauliwa; dawa za kulevya; umasikini; miundombinu mibovu; ukosefu wa haki katika jamii; huduma mbovu za jamii; viongozi wengi wasiofaa; n.k.

Na ukweli bado unabaki palepale, kuwa wageni (hasa weupe) bado tunaendelea kuwatukuza (kama mababu zetu walivyowabeba kwa machela) kwa kuwapa mikataba minono huku tukimkandamiza mzawa (Hivi jamani Idd Simba yuko wapi na sera yake ya uzawa?); mazingira ya uwekezaji yanampendelea zaidi mgeni kuliko mwenyeji. Mkiwa na ugomvi (wa kibiashara au kimaslani) na mgeni, ujue wewe mwenyeji umeumia. Tunawatetemekea mno hawa wageni.

Tazama tunavyoburuzwa kuingizwa kwenye Shirikisho la Afrika ya Mashariki!!! Jamani, hivi kweli tunalihitaji hilo katika muundo huo ili tupate kupiga hatua za maendeleo? Hatuwezi kubaki Watanzania na hadhi na heshima na uhuru wetu kama tulivyo na wakenya nao wakabaki walivyo, na waganda, na wanyarwanda, na warundi na basi tukaendelea kushirikiana katika biashara mpaka tuwe na rais mmoja?

Utumwa haujaisha. Kubeba mizigo hakujaisha. Kuwabeba wageni hakujaisha. Minyororo haijakatwa. Kudondoka na mzigo mkubwa mlimani bado kunaendelea. Ukombozi bado.

Tusipoangalia, itatuchukua WaAfrika miaka mingine 1000 kabla hatujafikia hadhi na heshima ya kuwa Watu wenye UTU.

Ciao!!!