Saturday, December 23, 2006

Nawatakia Krimasi Njema!


Wapendwa Wasomaji, ninachukua nafasi hii kuwatakia wote Krismasi Njema! Japo ni sikukuu ya kusherekea kwa kupeana zawadi, kula mlo mzuri na wa fahari, kukutana na familia na marafiki, kunywa pombe etc., tusisahau kuwa ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Napenda sana kipindi hiki Marekani, maana watu wanakuwa na roho nzuri na kusalimiana na watu ambao kawaida wasingewasalimia. Pia watu wanatoa misaada mingi kwa wasiojiweza na maskini kwa vile wameingiliwa na 'Christmas Spirit'. Hata bosi mwenye roho mbaya anaweza kuwa na roho nzuri japo kwa siku moja!

Wengine wataenda kwenye mikesha kanisani, wengine wataenda kwenye party, wengine watalala na kupumzika, wengine hawatasherekea kabisa hasa wasio waKristo.

Bila kujali dini, ninawatakia wote Krismasi Njema, na mapumziko mema.

Mungu Awabariki Wote!

4 comments:

John Mwaipopo said...

NAMI NAKUTAKIA HERI YA KRISIMASI NA MWAKA MPYA. HUU TUNAOUMALIZA (KAMA TUTAUMALIZA VEMA) UISHE SALAMA NA UTAKAOKUJA 2007 (TUKIUFIKA) TUENDELEZE YALE YALIYO MEMA, TUSAHAU YALIYOKUWA MABAYA, TUSAMEHE YALIYOTUKWAZA HUKO NYUMA.

MUNGU UWE NASI

MICHUZI BLOG said...

SAME TO YOU TOO. HOPE ALL IS WELL AND I STILL DONT BELIEVE HATUKUONANA ULIPOKUJA BONGO. VIJANA DAILY NEWS WANAKUKUMBUKA KWA BONGE LA LEKCHA ULOWAPA.

HAPPY CHRISTMASS!

mloyi said...

Tumeipokea kwa sababu tumeisikia tuu! haimaanishi kwamba wote tunaiamini, lakini bado ni jambo zuri kuwapa wenzako heri ya krismasi, nami nasema, Heri ya krismasi dada swahili times!

luihamu said...

Wengi hatukubali ukweli,ya kwamba hakuna uhusiano wowote ule kati ya krismasi na mila za watu weusi,tumeiga na tunaendelea kuiga kila siku.Waafrika tunamajukumu makubwa yanayo tukabili sio tu kufikiria krismasi.Jah live.