Monday, January 07, 2013

Cheka na Kitime Blog

www.chekanakitime.blogspot.com



NAWAKUMBUSHA TU JAMANI----- Naitwa John Kitime, nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza ‘bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, maana baada ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto wachanga. Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya kuchekesha, kama vile watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, na kilabuni, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na vyuo mbalimbali nchini na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na huko nilikutana na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua kuchekesha wakijitahidi kuchekesha, cha kushangaza si nikakuta wengine hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho cha kuchekesha wachekaji.

Katika kiota hiki cha www.chekanakitime.blogspot.com , ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.

Pia mimi ni mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui kucheza, hasa Chacha ndio kabisa halafu siku hizi kuna hii inaitwa Kwaito, wakati najitahidi kujifunza imeanza Azonto, jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio mbadili? Halafu huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?

No comments: