Tuesday, January 15, 2013

Profesa Jay aka. Joseph Haule Yu Hai - Hajafa!

Wadau, leo habari zilisambaa kwa kasi kuwa mwimbaji, rapper Profesa Jay aka. Joseph Haule, alizimia na kufa hapo papo.  Asante Twitter na Facebook habari hiyo ya uwongo ulisambaa kwa haraka.

Nafurahi kuwaaambia kuwa hiyo habari si kweli.   Profesa Jay yu hai na anawasalimia.  Namtakia Projesa Jay maisha marefu.

Jamani, acheni tabia mbaya ya kuzusha habari zisizo kweli!

3 comments:

Anonymous said...

Wabongo bwana. Sasa ndo yamekuwa kwa yale mambo ya Will Smith kafa Switzerland etc.! Duh!

Anonymous said...

Wabongo wengi wako 'idle' ndio maana wanaanzisha uzushi wa kipuuzi kama huu.

Anonymous said...

Nakumbuka haya mambo ya kuzushiana kifo yalianza mwaka 1983 uliposambaa uvumi jijini Dar kuwa Ndala Kasheba amefariki dunia.