Tuesday, November 12, 2013

Tangazo La Philips Redio - Miaka ya 70-80

Wadau mna kumbuka ile tangazo kwenye Radio Tanzania enzi zile: watoto walikuwa na vikundi wanashindana kuimba.  Shule walimu walikuwa wanachukia maana darasa nzima inaweza kuimba. Hizo redio zilikuwa mali kweli, tena kabla ya TV kuruhusiwa.

Philips 
Ndio enyewe
Sauti Safi
Sauti Kubwa!


2 comments:

Baraka Mfunguo said...

DUDUPROOF ilikuja kufunika baadae. Hizi ndizo zilikuwa siku najaribu kupata picha lakini ndio hivyo wakati ukuta. Ukipita haurudi

Baraka Mfunguo said...

DUDUPROOF ilikuja kufunika baadae. Inasikitisha kuona jinsi viwanda hivi vilivyokufa haijalishi kama ni assembling industries ila vilikuwa ni sehemu ya maisha ya watanzania. Chukulia Matsushita pale Pugu road waliokuwa wakizalisha NATIONAL.

Kulikuwa mpaka na bendi ya NationalPanasonic. Ni kumbukumbu nzuri sana .