Saturday, February 14, 2015

Mwanamke Mweusi Maskini Ashinda Bahati Nasibu Powerball - Atapata Dola $188M

Marie Holmes (26) Mmoja wa Washindi watatu wa Powerball
Wadau, hatimaye mtu maskini mwenye shida kashinda bahati nasibu.  Mwanamke mweusi na maskini mwenye watoto wanne, Marie Holmes (26) ni mmoja wa washindi wa tatu wa Donge Nono la Powerball.  Zawadi kuu wiki hii ilikuwa karibu dola $600 milioni.  Wameshinda watu watatu na watagawana hivyo atapata dola $188 milioni.  huyo mama alikuwa anafanya kazi zilizokuwa zinamlipa kima cha chini. Ana watoto wanne na mmoja ana ugonjwa wa Cerebral Palsy inayoathiri ubongo. Anasema maisha yake ilikuwa ya dhiki. Nafurahi kuwa sasa yeye na watoto watakuwa na maisha mazuri na kuweza kusoma hadi Chuo Kikuu bila kuogopa gharama. Mungu ambariki.

Washindi wengine wanatoka mikoa ya Puerto Rico na Texas.

Kwa habari kamili BOFYA HAPA:

2 comments:

Mbele said...

Hongera zake. Lakini awe makini sana, kwani wako ambao walipata fedha nyingi sana katika hizi bahati nasibu halafu wakaja kufilisika. Sijui afanyeje ili yasimkute hayo.

Anonymous said...

Ana watoto wanne au watatu? Unatuchanganya Chemi.