Tuesday, February 03, 2015

Mshenzi aua Mke Wake Hotelini Manzese!

Hii hatari sana!! Mwanaume anayejulikana kwa jina la Remy Joseph (35) anashikiliwa na polisi kwa kumchinja mke wake wa ndoa kabisa aitwaye Josephine Ndengaleo Mushi waliyeishi naye miaka 10 na kuzaa watoto wawili. Tukio hilo la kutisha lilijiri ndani ya chumba kimoja kilichopo ghorofa ya pili ya Hotel Friend’s Corner Ltd iliyopo Manzese Argentina, Dar ambapo walikuwa wamechukua chumba katika hoteli hiyo kwaajili ya kulala hapo.
Polisi walifanya uchunguzi chumbani na kugundua kuwa, marehemu Josephine alichinjwa shingoni, akakatwa mbavu mbili, moyo na maini vilikuwa nje ‘vikimwagika’, mwisho alichomwa kisu utosini.. Cha kusikitisha zaidi, mwili wa marehemu Josephine ulipigishwa magoti, sehemu ya miguu mpaka magoti ikiwa sakafuni na kifuani kulalia kitanda. Halafu ulifunikwa shuka
Katika hali iliyoonesha kuwa, mtuhumiwa baada ya kutenda ukatili huo alitaka kujinyonga, polisi walikuta waya wa umeme wa tivii ukining’inia kwenye pangaboi lakini ukiwa umekatika. Na pia damu na alama za kujikata visu shingoni.
Sababu ya kufanya hivyo haijujulikana ila ndugu wa mke wa marehemu walielezea kuwa mme alikuwa akimhisi vibaya mkewe.
R.I.P Josephine Mushi

2 comments:

Anonymous said...

Wanaume wote tuombe mungu atunusulu na mambo hayo,kweli mapenzi yanauma lakni ukimuua mtu unaempenda ndio utamaliza matatizo yako?? tukae chini tuongee na wapenz wetu ikishindikana tuachane nao tu!

Remmy Jr. said...

Maumivu ya Mapenzi huchoma sana moyo. Ni maumivu ambayo huwezi fananisha na chochote. Akikupenda mtu mpende kama humpendi ni heri umwambie wazi sio kumdanganya na kila siku kumpa moyo kumbe una mcheat. REMY JOSEPH anapaswa kuhukumiwa na MAHAKAMA YA MAPENZI ila si hizi mahakama za kawaida. Huyo JOSEPHINE MUSHI ni mmachame siwezi sema wala kuhukumu kua alistahili hiyo adhabu ila wanawake wakimachame wanajulikana USIPOMUUA WEWE ATAKUVIZIA YEYE.! MAJUTO NI MJUKUU and TAKE CARE WITH SOMEONE HEARTS. MAUMIVU YA MOYO HASA JUU YA MKE YANAUMA SANA.