Sunday, March 29, 2015

Watanzania - Wakimbizi Ulaya!

 
Malazi ya Wakimbizi huko Ujerumani


Nimepata kwa E-Mail:

 Hivi karibuni nilikuwa safarini Nchini Ujerumani. Na moja ya mambo niliyoyakuta ni kwamba siku hizi nchini humo kumefunguliwa makambi sehemu mbali mbali ya wakimbizi. Wengi wao ni kutoka nchi za Afrika. Nadhani mnasikia mara kwa mara kuhusu wakimbizi hawa ambao huenda Ulaya kwa njia ya hatari ya Meli. Wengi hufa bahari kwa hali mbaya ya hewa au hata kwa kutoswa.

Nchini Ujerumani nilikuwa katika Jiji la Munich. Nilibahatika kuona moja ya kambi hiyo, ila kwa bahati mbaya sikuruhusiwa kuingia. Niliambiwa kadiri ya orodha yao kuna WATANZINIA WAWILI. Nilipopata habari hiyo nilishituka sana. Hata aliyenipa habari hiyo aliona sikuwa tena katika hali ya kawaida. Ndipo akaniuliza nchini kwenu kuna matatizo gani hata watu wakimbie huko? Hakika sikuwa na jibu. Sababu za ukimbizi nchini mwako zinaweza kuwa za Kisiasa, yaani kutokana na utawala mbovu watu wanaamua kukimbia kuokoa maisha yao. Au hali hali nyingine yoyote inayohatarisha maisha. Mimi ninajiuliza nchini Tanzania kuna hali gani ya kuhatarisha maisha ya watu hadi wakimbie wakaishi kwenye makambi Ugaibuni? Hakika nilisikitika sana.

Ila kwa vyovyote wanazo sababu zao za kimsingi kukimbia na hata kujiorodhesha kama wakimbizi. Wito wangu kwa vijana; hakika wengi wanadhania Ulaya ni sehemu poa. Kuna fedha za kumwaga na maisha huko ni rahisi. Kiukweli ni kujidanganya. Hapa Tanzania unaweza kwenda sokoni ukaokota hata matunda au mbogamboga ukaponea. Ukafanya kibarua chochote kitu hata kufanya usafi kwenye zizi au bustanini au hata kuiba kwa wale wenye ujuzi huo. Kwa wenzetu hayo hayapo. Hakuna cha kibarua. Hakuna mazingira unayoweza kuiba kirahisi. Kila duka na soko kuna makamera. Hali ya hewa ni mbaya. Muda mwingi katika mwaka ni baridi kali. nk. Witoa kwa vijana kama unataka kuteseka maisha yako yote kimbilia Ulaya.

Walioko kule wako makambini. Hawaruhusiwi kusafiri, hawaruhusiwi kufanya kazi ila wanafugwa tu kwa kupatiwa chakula na mahitaji mengine ili waishi. Wanangoja ufanyike utaratibu wa kurejeshwa makwao. Je huko si kupoteza muda na kuhatarisha maisha zaidi. Kinachoniuma zaidi ni je, hapa Tanzania kuna mazingira gani magumu kiasi hicho hata wajiorodheshe kuwa wakimbizi? Kama kuna mwenye maelezo ya sababu ningeshukuru.

K

6 comments:

Anonymous said...

Niliyosimuliwa mimi na mama mmoja ambapo alifukuzwa kazi kampuni ya Benz ofisi ya UK kwa kumwatukana wazungu yalinisikitisha. Pia nilishawahi kurudi ktk ndege moja na kijana aliyekuwa amerudishwa kwa nguvu toka nchi moja ya ulaya nikampa hata nauli ya bus alikuwa hana hapo airport. Huko UK 2009 huyo mama alieleza kudhalilishwa vijana wanaotoroka na kuhamia huko. Ili wapate kazi/ajira huko na kudumu ktk kazi hufanyiwa vitendo vichafu na hao wazungu. Nchi nyingine hunyang'anywa passport na hela hukaa na tajiri kwani hawezi kufungua account hana social security number. Akimkorofisha boss-hutoa siri, anakamatwa, anarudisha bila ya senti hata moja zilizokuwa zinakaa kwa boss. Maisha hayo magumu lakini bora yupo ulaya. Ukipita kona unaongea kiswahili wanaojibanza vijumbani wakikusikia wanakudandia kukusalimia na kutaka kujua unakaa wapi. Ukiwaonyesha hawabanduki kuja kuomba hiki na kile-njaa kali shida tupu. Wadada wanachafuliwa pia wakaka wengine wababa na
familia zao kwao. Bora ufie melini kuliko kulima na kuuza nyanya ngerengere mabonde ya mto Ruvu. Chunga pia hapa nchini kutafutia watoto wako wa kiume na kike wasio na ujasiri na uelewa kazi katika makampuni binafsi ya wageni na wenyeji. Hata kazi za kufagia barabara na kuzoa taka tumekuta simulizi ya ajabu ni chafu kama zilivyotakataka zenyewe. Rushwa ya ngono imepamba moto pamoja na HIV/AIDS kuwa janga la dunia. Ukubali au ukose kazi au utolewe kazini. Mungu anisamehe lakini nimefanya research na kutembea na wazoa taka na wafagiaji DSM mwaka 2003 jioni na usiku mpaka saa 8 nikajionea mengi. Pia utafiti wa sexual abuse umenionyesha mengi na utafiti wa mashoga-ni kioo katika maisha yangu wanapoeleza ilikuwaje, alianzaje, na nani na anapangiwa nyumba na mtu wake ni nani. Dunia imekwisha.

Mbele said...

Huwa nasoma maandishi ya Albert Sanga na Meshach Maganga, ambao ni wajasiriamali walioko Tanzania. Hao ni watu wanaojituma sana katika kujielimisha. Meshack Maganga, kwa mfano, ananunua na kusoma sana vitabu vya maendeleo na ujasiriamali.

Hao watakuAMBIA kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi sana. Na wao wenyewe wana. Makala ya hivi karibuni ya Albert Sanga niliyosoma inasisitiza kuwa ajira ziko tele Tanzania, kwa yeyote mwenye macho.

Watakuthibitishia kuwa hakuna sababu ya watu kuikimbia Tanzania kwa sababu za kiuchumi.

Haya ni mawazo ya hao wajasiriamali, ambao ni watafutaji wa elimu bila kuchoka na wanatekeleza hayo wayasemao kwa ufanisi mkubwa.

Labda nimalizie kwa kusema kuwa wa-Tanzania wenye sababu ya kuikimbia nchi ni albino, ambao maisha yao yanatishiwa na kuhujumiwa usiku na mchana na jamii iliyojaa ushirikina, isiyostaarabika, na pia serikali isiyowajibika ipasavyo.

Anonymous said...

Ndugu zangu, "kitanda usichokilalia hujui kunguni wake". Tanzania mwieha magumu kwa sababu nyingi mno. Wananchi hawana elimu ya kutosha khs ujasiriamali na pia hakuna wa kuwawezesha. Mwananci wa kawaida mwenye amejitahidi kufikiria kuhusu biashara atakuambia kuwa anafikiria kuuza makaa, vitafunio km maandazi, chapati nk, hao ni kwale wanaoishi mjini ambapo hawawezi kujiwekeza kwenye kilimo. Sasa kundi hili ni ngumu hata kusomesha watoto wao, kwanza hawana ushawishi kuhusu elimu na hata wakiwa nao huo ushawishi hawataweza kujiendeleza kutokana na ugumu wa maisha.
Na wanaliopo vijijini pia wanakosa dhana muhimu, ndioa mana wanakufa njaa.
Vyama vya mikopo vinasaidia lkn interest ni kubwa mno, sasa kwa biashara ndogo ndogo wanakuwa hawafiki mbali kwa sababu ni km wanawafanyia kazi hayo makampuni.

Serikali imewatupa wananchi wake mno, hakuna ajira mpya zlizoilozokuwa created, changamoto za maisha zinawafanya wananchi kukata tamaa. Leo hii mtu akiwa malaria hawezi kumudu gharama za matibabu, huu ni mtihani mkubwa kwa taifa.

Kwa waliosoma nao ni tatizo, tunarudi pale pale kuwa ajira hakuna. Mtu amemaliza chuo kikuu anakaa nyumbani miaka hata mitano hapati kazi, kazi ni za kujuana au hongo ambapo wananchi wengi hawamudu.

Kwa nchi zilizoendelea ni tofauti ajira ni nyingi na serikali zipo kwa ajili ya wananchi wake sio families zao.
Kikwete anakazi ya kwenda kutoa pole tuu wananchi wakipat maafa, lkn hafikirii jinsi ya kuboresha maafa yasijirudie. Hajui kuadabisha viongozi wanapokosea. Mfano mzuri suala la ESCORW, liketokea km hilo nchini Kenya na rais wao ame respond km inavyotakiwa. Viongozi wote karibu 70 wamesimamishwa kazi bila malipo kupitisha uchunguzi, lakini leo hii Tanzania yetu wala Rushwa km kina Lowasa walioitia nchi ktk maafa wanapigiwa debe wawe viongozi wa juu, huu ni mtihani mkubwa kwa taifa.
Pesa wana zopoteza kwenye campaign zingesaidia mahospitalini, ambapo wananchi wanakosa huduma bora


Mm nafikiri serikali imerundika viongozi wasio na exposure yoyote, wanateua kw kujuana. Laiti serikali ta Tanzania ingeibadili mfumo wake, basi nchi ingepiga hatua sasa

Anonymous said...

MAAGENT WANAWADANGANYA KWA KULA YAO.
KUNA NCHI ZA EUROPE MFANO ITALY,BURGARIA AMBAZO ZIKO KWENYE UMASIKINI.
WAKIMBILIE NCHI TAJIRI NA SIO KUZAMIA WAWE NA KESI ZITAZOWAWEKA NCHINI.
GOOGLA UONE MKIMBIZI AKIWA SWED,DENMAR NK ANALIPWA KULIKO MFANYAKAZI WA FULL TIME

TANZANIA KWETU ANGALIA WIMBO WA MRISHO MPITO "NJOO UICHUKUE" NDO UTAJUA WATANZANAIA WENGINE WANAISHI VIPI TANZANIA.
TANZANIA WENYE MAISHA NI WALE WENYE ELIMU NA WENYE CHANEL NZURI.
SISI TUNAMATAJIRI NCHIN ILA BADO HATA MTU AKIUMWA TUOMBE MCHANGO TIGO ILI ATIBIWE. NA WAKO WENYE HELA MPK HAWAJUI WAZIFANYIE NINI

INGIA MUHIMBILI ONA WAGONJWA TENA NENDA HODI YA WATOTO NDO UTAONA AFADHALI NIISHIULAYA KAMA MNYAMA KULIKO KUZALIWA MASIKINI TANZANIA (AFRIKA)

NAIPENDA NCHI YANGU NA NASIKITISHWA NA WAZAMIAJI WANAOENDA NCHI ZISIZO NA SHERIA AU WANAZAMIA PAHALA BILA KUJUA NINI MBELE .
MTU ANAZAMIA MFANO MAREKANI,UFARANSA WAKATI KUNA SEHEMU HAZITFAUTIANI MNA TANZANIA KWA KUCHOKA.
KIMBILIA NCHI KAMA SWEDEN UONE MKIMBIZI ANATHAMINIWA VIPI NA UKIWINI KESI NDO UTATAMANI UNGETOROKA NA FAMILIA NZIMA.

KUHUSU SWALA LA KUNYANYASWA NIMESIKIA ILA NADHANI WANANYANYASWA NA WEUSI WENZAO WALOWABEBABILA MSAADA . SIJAWAHI KUSIKIA MWAFRIKA KAJA HANA KIPANDE APATE KAZI KWA MZUNGU ZAIDI YA KAZI YA KUFAGIA MAOFISINI TENA UWE NA MTU ANAYEISH AKUUNGANISHIE.

SIO UTAPATA TUU HAKUNA LABDA NCHI ZENYE SHERIA INAYOFANAN NA TANZANIA.
MANYANYASO MENGI HUPATA NCHI ZA KIARABU, TURUKIA AU NCHI ZA ULAYA ZILIZO KATA HESABU YA NCHI ULAYA MASIKINI.

MIE NARAFIKI ANAFANYA KAZI YA KUTAFSIRI ,AKIJA MKIMBIZI KUTOKEA KENYA AU SOMALIA AU MOMBASA HUWA WANAWINI.
KUHUSU UKIMWI NADHANI WANAUFWATA KWENI NCHI NYINGI ZA ULAYA UKIMWI WAUGUAJI WACHACHE KWANI UKIMWAMBUKIZA MWENZIO UKIMWI AU UGONJWA WA ZINAA UJUE UTATUMIKIA JAENA .
NA YEYETE MWENYE UKIMWI AKIWA KAZAMIA AKAJIPELEKA KWA AJILI YA UKIMWI UJUE ANABAKI NA ANAPEWA VIZA.

MIE NIKO KTK CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WEUSI EUROPE NACHOANDIKA NAJUA KINAENDA VIPI

NGAZI ZA JUU WANGEFUNGUA MAOFISI HATA YA KUFUTA MEZA ILI WATU WAPATE AJIRA NYUMBANI .
SIE TUNAOANDIKA HAPA NI WOTE WNYE UWEZO WA KWENDA KAFE NA KULIPIA INTERNET AU TUNA LAPTOP NYUMBANI TUSISAHAU KUNA MTANZANIA HAJALA TOKA JANA ,ANAYEJIUZA BUGURUNI ALISHE FAMILIA.
MSIKILIZE MRISHO UTAONA MAISHA YA MTANZANIA YAKO WAPI

Anonymous said...

Watu wenye roho mbaya bwana utawajua tuu.
Wanapata hasira sana kuona watu wakichakarika utafuta maisha kivyao. Mtu akiomba ukimbizi Munich wewe inakuhusu nini?

Ondoeni roho zenu za kunguni hapa.

Hawa watu wa kutoka shamba kama huyu anayejiita profesa mbelu nyuma ni wajinga kiasi kwamba wanadhania haki ya kuishi ulaya ni ya wao peke yao na vidigrii vyao vya manzese univesti.

Anonymous said...

WEEEE!!!!! ANON WA aPRIL 01.2015 6:08NPM KULA TANO UMENIKOSHA SANA, WENGINE MAISHA YAMEKULA KWAO BASI HAA WANASAHAU HATA WALE WENYE SHIDA, TANZANIA NI MATATIZO, MTU HAWEZI KIMBIA TUU HIVI HIVI KWAO KUKIWA MABO POA. HAO WENGINE WALIOTOKA SHAMBA NA VIDIFREE VYAO VYA MANZESE MICHOSHO MITUPU, WAFANYE LICECHI KWANZA KABALA YA KUANDIKA HAPA FREEDOM OF SPEECH WAONE MAISHA YA WATANZANIA,HAWANA HATA POSIBILITIES WALIO WENGI