Thursday, November 19, 2015

Mwanahabari Nashon Kenedy Awapa Siri Ya Mafanikio Wasanii wa Mwanza

Kulia ni Mwanahabari Nashon Kenedy kutoka gazeti la kiswahili la Habari Leo na lile la kiingereza la Daily News akiongea katika hafla ya kuzaliwa kwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss ambae ni Mtengenezaji wa Filamu katika Kampuni ya Shafineyz Film Production ya Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Mwanahabari Nashon Kenedy kutoka gazeti la kiswahili la Habari Leo na lile la kiingereza la Daily News amewashauri wasanii wa maigizo Jijini Mwanza, kubadilika na kuigiza filamu zinazogusa maisha halisi ya Kitanzania na kuachana na uigizaji wa filamu zisizo na uhalisia wa maisha ya Kitanzania hususani filamu za mapenzi. 

Kenedy aliyasema hayo jana katika hafla ya kuzaliwa kwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss ambae ni Mtengenezaji wa Filamu katika Kampuni ya Shafineyz Film Production ya Jijini Mwanza ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo pamoja na wageni wengine, pia ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu kutoka Jijini Mwanza.

"Japokuwa maisha yetu yanategemea mapenzi, lakini mimi nawashauri kwamba acheni kuigiza filamu za mapenzi kila siku kama mnahitaji kufanikiwa. Igizeni filamu zinazoeleza maisha halisi ya kitanzania kama vile kuonyesha matatizo yanayowakabili wananchi, na hapo ndipo mtaweza kuwa tofauti na waigizaji wengine jambo ambalo litawasaidia kufikia katika mafanikio yenu". Alibainisha Kenedy.

Katika hafla hiyo, Kisiba aliwashukuru wale wote walioungana nae katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo aliahidi kuitimiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa soko la uigizaji wa filamu Jijini Mwanza linafufuliwa kupitia Kampuni anayofanyia kazi ya Shafineyz Film Production kwa kuwa ni aibu kukosekana kwa soko la filamu Jijini hapa ikilinganishwa na majiji mengine nchini kama vile Jiji la Dar es salaam. 
Tazama HAPA Picha za Hafla hiyo

No comments: