Monday, May 09, 2016

Tanzia - Maggid Muhidin (Mtoto wa Kaka Michuzi)

Ankal Issa Michuzi anasikitika kutangaza kifo cha mwanae Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini, alikokuwa masomoni.

Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu inafanywa, msiba utakuwa Tabata Mawenzi jijini Dar es salaam ambako ratiba ya mazishi itatoka mara tu baada ya mwili kuwasili.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

Innalillah wa inna ilayhi raajiun

2 comments:

Freddy Macha said...

Poleni sana familia ya Michuzi. Inauma sana. Tupo nanyi katika sala zetu.

Anonymous said...

Rest in peace Maggid Muhidin. CONDOLENCES to the Michuzi family.