Saturday, May 13, 2017

Tanzia - Mh, Said Thabith Mwambungu

 
The late Regional Commissioner Said Thabith Mwambungu
 
Kutoka kwa mwandishi mahili  Nickson Mkilanya 
 
 KWAHERI YA KUONANA RC SAID THABITH MWAMBUNGU
 
Amefariki leo katika hospitali ya taifa ya muhimbili,hatunaye tena, Said Thabith Mwambungu mkuu wa mkoa mstaaf na miongoni mwa wanasiasa wabobezi na wakongwe katika zama hizi.
Ameripotiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa figo kwa siku kadhaa hata akapelekwa kutibiwa nchini India na kurejea na nafuu ambayo pia haikupata kumrejesha katika majukwaa ya siasa na hata hadharani.
 
Kuugua huko pasipo kutajwa kuwa ndiyo sababu iliyopelekea rais Magufuli kumhamishia ofisi ya waziri mkuu na kuahidi kumpangia kazi zingine toka juni 26 mwaka jana lakini nafsi yangu yakiri kuwa pengine hiyo ndiyo sababu kuu.
 
Alilitamka kwa ufasaha jina lake la said said thabith mwangu enzi za uhai wake hasa pale nilipofanyakazi naye mimi nikiwa kama mwanahabari wa luninga,radio na hata magazeti, ni mzaliwa wa Malinyi mkoani Morogoro ambaye kwangu mimi ni miongoni mwa wanasiasa bora,baba Bora na kielelezo cha watu wema na wastaarabu niliopata kukutana nao.

Miongoni mwa mambo aliyoyaacha km funzo kwangu ni uvumilivu na upendo. Wakati mmoja akiwa mkuu wa wilaya kuna kiongozi mmoja alimfanyia figisu figisu nyingi ambazo hata wanahabari tuliona na kugundua akionewa dhahiri! Lakini tulipoongea naye jibu lake alijibu kuwa mwacheni tu huyo, hayo ni yakupita, hajui siasa, vumilieni yataisha na kweli huyo mtu alikuja ondolewa ktk nafasi na kumwacha mwambungu akitamba na siku chache baadae kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa ruvuma.
 
Jambo lingine alijua kuthamini watu na kuwaonesha upendo wa dhati hata wale ambao kwa tabia za kibaguzi wasingepaswa kumsogelea lkn bado aliwapa nafasi sawa na wale ambao kimtazamo walikuwa na sifa ya kumsogelea. Nakumbuka wakati mmoja aliniambia nick mwanangu fanya mpango uoe nikufanyie sherehe kabla sijaondoka na hapa alimaanisha kabla hajahamishwa kituo cha kazi nami nilicheka na kuahidi kufanya hivyo lkn leo hatunae tena ameondoka mwambungu pasipo kushughudia harusi yangu.
 
Amini mungu ni mwema wanae wakiongozwa na hamidu mwambungu watashughudia harusi yangu kwa niaba yake inshallah.
 
Wakati wa uhai wake alipata kuwa kada mwandamizi katika ccm, katibu wa chama cha mampinduzi mkoa,  mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa achilia mbali nafasi zingine nyeti ndani ya nchi hii, Na ameacha watoto watatu, hamidu said said thabith mwambungu, Khalid na Abiba S. S Thabith mwambungu na mjane.
 
 Mtoto mkubwa wa marehemu  aitwae Hamidu Mwambungu anasema haijaamuliwa bado kama baba yao atazikwa morogoro au kwingineko.
 
Tangulia mtu mwema Said Said Thabith Mwambungu.

2 comments:

Tom olali said...

Nice article.Congratulations

Tom olali said...

Rambirambi zetu kutoka idara ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Nairobi..Unaweza ukatupa katika tovuti http://kiswahili.uonbi.ac.ke/