Saturday, May 27, 2017

Ucheleweshaji wa Pembejeo Umetajkwa Kuporomosha Kilimo Mkoani Geita

UCHELEWESHAJI WA PEMBEJEO UMETAJWA KUPOROMOSHA KILIMO CHA PAMBA WILAYANI MBOGWE MKOANI GEITA


Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbogwe, (kulia), Elias Kayandabila, akizungumza  na waandishi wa habari, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani Geita kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi 
akizungumza na ujumbe huo.
Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya Mbogwe, Stephen Shilemba, akizungumza katika mafunzo ya siku moja ya maofisa ugani yaliyoendeshwa na COSTECH na OFAB.
Maofisa Ugani wa Wilaya ya Mbogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania, Philbert Nyinondi (kushoto), akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe, Christopher Bahali (katikati), akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya mkurugenzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani humo, Deus Lyankando na Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilayani humo, Deus Lyankando na Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza katika mafunzo hayo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Amina Kanyogoto.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya hiyo, Vicent Busiga (kulia), akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mtaalamu wa mazao ya mizizi kutka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru Mwanza, Dk.Simon Jeremiah akitoa mada kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo.
Mtaalamu wa magonjwa ya  pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiliguru, Stellah Chirimi (kulia), akitoa mada.




Mkulima wa pamba, Magua Mayala (kulia),mkazi wa  Kitongoji cha Kakumbi Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe mkoani Geita akizungumza na waandishi wa habari jana, walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani humo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.
Mkulima wa Kijiji cha Kakumbi, Said Tangawizi (kushoto), akiwaonesha maofisa kilimo hao eneo ambalo linafaa kwa shamba la mihogo la mfano.
Mkulima wa Kijiji cha Kakumbi, Said Tangawizi (kushoto), akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo cha mhogo, mpunga,mahindi na viazi lishe.
Watafiti na wanahabari wakitoka kuangalia shamba la mpunga la mkulima, Said Tangawizi. Wa kwanza kushoto ni Mshauri wa OFAB, Dk.Nicholaus Nyange, Stellah Chirimi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiliguru, Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF nchini Kenya, Suleiman Okoth, Mwandishi wa Habari, Fatma Abdu na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJAF), Gelard Kitabu.

Na Dotto Mwaibale, Mbogwe

KUCHELEWA kufikishwa kwa pembejeo za kilimo kwa wakati kwa wakulima wa pamba imeelezwa kuwa kunachangia kuporomosha kilimo hicho wilayani Mbogwe mkoani Geita.



Hayo yalielezwa wilayani humo jana na Magua Mayala, mkulima wa pamba wa Kitongoji cha Kakumbi Kata ya Lugunga wilayani Mbogwe mkoani Geita wakati akizungumza na waandishi wa habari walioongozana na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) pamoja na Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) waliopo mkoani humo kwa ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani.

Mayala alisema changamoto kubwa waliyonayo wakulima katika wilaya hiyo ni kucheleweshewa pembejeo hali inayowafanya waende kutafuta mbegu ambazo hazina ubora ambazo zinawasababishia wakulima kupata mavuno kidogo ukilinganisha na maeneo ambayo wanapata mbegu bora.

"Tunaiomba serikali itusaidie kutufikishia pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuliinua zao la pamba ambalo ni la biashara katika wilaya yetu" alisema Mayala.

Alisema alipanda ekari moja ya pamba kwa kutumia mbegu duni ambapo alipata kilo 100 alizouza sh. 200,000 na kueleza kuwa changamoto kubwa ni pamoja na dawa za kuulia wadudu waharibifu wa pamba na hata wakipata dawa hizo haziui wadudu.

Mtaalamu wa magonjwa ya mazao hasa ya pamba kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Ukiliguru, Stellah Chirimi aliwataka wakulima kuzingatia kilimo chenye tija kwa kufuata maelekezo ya wataalamu na kuachana na kilimo cha mazoea.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe, Christopher Bahali aliwataka maofisa ugani wa wilaya hiyo kwenda kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo na kuwaelekeza badala ya kukaa mjini jambo ambalo litaongeza uzalishaji wa chakula.

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Vicent Busiga aliwapongeza maofisa ugani kwa jitihada zao wanazofanya za kuwafikia wakulima licha ya kukabiliwa na changamoto ya umbali wa kutoka eneo moja kwenda lingine kutokana na kukoseka kwa usafiri.


Mshauri wa Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange alisema matumizi ya teknolojia ya bioteknolojia katika kilimo ni muhimu kwani katika nchi za wenzetu wanaoitumia kama, Mali, Burki Faso na Misri zimepiga hatua kubwa.

"Nchi kama Burkina Faso imepiga hatua kubwa ya kilimo cha zao la pamba baada ya kuamua kutumia mbegu zenye vinasaba (GMO), ambazo Tanzania hazikubaliki na hivi sasa inazalisha wastani wa tani 2.9 kwa hekta ambapo nchi zote za Afrika zinakwenda kujifunza kwao kuhusu kilimo cha pamba" alisema Nyange.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)



No comments: