Thursday, July 13, 2017

TRA Waifungia RFA Kwa Kudaiwa Kodi ya Sh. Bilioni 4.5

Mamlaka ya mapato Tanzania inadaiwa kuifungia Radio Free Africa ya Mwanza inayomilikiwa na Antony Dialo kutokana na kudaiwa kodi kubwa.

TRA wamewaondoa studio wafanyakazi wote na kuifunga radio hiyo. Kwa sasa ukiwasha radio utasikia matangazo ya kiingereza ya BBC.

Diallo ni mwenyekiti wa CCM Mwanza na anadaiwa mamilioni ya kodi na TRA miaka mingi.

Star TV pia imekumbwa na sekeseke hilo. Ikumbukwe hii ndio TV pekee binafsi iliyokuwa ikipingana na MOAT na TEF katika sakata la RC Paul Makonda na walirusha kipindi maalum cha Makonda huku Jumuiya ya Wanahabari wakitangaza rasmi kujitenga na maswahibu yoyote yatakayokuja kuikuta RFA na Star TV.
https://www.jamiiforums.com/th reads/tra-waifungia-rfa-kwa-ku daiwa-kodi-ya-sh-bilioni-4-5. 1283386/page-11#post-22223509

No comments: