Showing posts with label AIDS. Show all posts
Showing posts with label AIDS. Show all posts

Saturday, June 11, 2016

Watoto waliozaliwa na Maanbukizi ya VVU (HIV) Wataka Jamii Kuwakumbuka!

Imeelezwa ili kuwawezesha watoto yatima ambao walizaliwa wakiwa na Virusi vya UKIMWI ambao wanapatikana katika Kituo cha Matumaini kilichopo Manispaa ya Dodoma, Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao ambao wanaishi katika kituo hicho ili kuwawezesha kuishi mazingira bora pamoja na kupata huduma za bora za afya.

Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo, alisema kituo hicho chenye watoto 151 wakati kimeanzishwa kilikuwa kikipokea msaada kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na TACAIDS lakini kwa sasa msaada umesimama na hivyo kuwafanya kwa sasa kuishi katika mazingira magumu.

Sister Maria alisema kuwa hali ya maisha kwa watoto hao ni ngumu na hivyo kuwataka Watanzania kuwakumbuka watoto hao ambao walizaliwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili waweze kupata huduma bora ambazo zitawawezesha kuishi katika mazingira bora, kupata elimu na kupata dawa ambazo zitaimarisha afya zao.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiongozwa na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo katika manispaa ya Dodoma karibu na Hoteli ya Mtakatifu Gasper.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

“Hapa wanakuja tu watu wa hapa Dodoma mara nyingi siku za Jumamosi na Jumapili ila tofauti na hivyo hatuna msaada mwingine, watoto hawa wanahitaji faraja kutoka kwa watu wengine inapendeza kuona watu wanakuja kuwaona na kuwasaidia nao wanafurahi,

“Ukiangalia hali ya kimaisha inazidi kupanda tunafanya jitihada kujisimamia sisi wenyewe lakini tunashindwa bado tunahitaji msaada sisi tumejitoa kuwasaidia hawa watoto hata hatulipwi lakini tunahitaji sana msaada wa Watanzania,” alisema Sister Maria.

Nae Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999 na Mtalaam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu ambaye alifika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada ambapo alituma ujumbe kwa Watanzania wengine ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kutoa misaada kwa wahitaji na kuwataka kubadilika.

Bi. Temu alisema kuwa mazingira ambayo wanaishi watoto hao ni magumu na hawana wazazi kutokana na wazazi wao kuwa wamefariki hivyo kuwataka Watanzania kujitoa kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao kwa chochote ambacho kinaweza kuwasaidia kuimarisha maisha yao ili waishi mazingira bora.

“Jamani kama watu wanasema tunapoishi kuna shida basi hakuna, shida zipo huku, ukiangalia kuna watoto wengine wana wiki moja na hawana wazazi wametupwa wanahitaji kupata misaada ya Watanzania,

Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimsikiliza kwa makini mmoja wa watoto wanaoishi kituoni hapo aliyewahi kumuona mara ya kwanza alipofika kituoni hapo.

“Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu kama una pesa au nguo au chochote ambacho kinaweza kuwasaidia tutoe kwa watoto hawa mazingira yao ni magumu sana, hawana makosa hawa hata mbele za Mungu naomba tuwasaidie,” alisema Bi. Temu.

Kwa yoyote atakayeguswa na angependa kufika kituoni hapo kusaidia anaweza kupiga simu kwa Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo +255754272707
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kulia) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiwa wamewabeba watoto yatima wanaoishi kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahia jambo mara tu baada ya kuwasili katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma kinacholea watoto yatima ambao 98% wanaishi na Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwa kwenye wodi ya watoto wachanga ambao ni yatima wanaoishi waliozaliwa na maambuki ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni pamoja na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo (kulia) walipotembelea wodi ya watoto wachanga waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahi na watoto wachanga ambao ni yatima waliozaliwa na maaumbikizi ya Virusi vya Ukimwi waliolazwa katika wodi ya watoto kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Wewe acheka afurahi kumuona Aunty....Jiji jiji jiji.....jamani acheka....Ni maneno ya Mlimbwende Hoyce Temu akicheza na mmoja wa watoto hao katika wodi hiyo.
Meneja Mwendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige akimbeleza mmoja wa watoto waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wanaolelewa katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Eweee Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, tunakuomba wajaalie Malaika wako hawa afya njema, maisha marefu, wape uponyaji viumbe hawa wasiokuwa na hatia, Amen!
Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo akimsimulia Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu historia ya mtoto Richard aliyeshikwa mikono na mlimbwende huyo.
Mmoja wa Masista wanaohudumia watoto hao Sista Mary Shayo akifurahi jambo wodini mbele ya kamera ya Modewjiblog.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akicheza kwaya ya wimbo maalum aliokuwa akiimbiwa na bendi ya kijiji cha Matumaini kabla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali.
Hoyce Temu akigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa kwenye kijiji cha Matumaini mkoani Dodoma.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi 'Pampers' kwa mmoja wafanyakazi wanaohudumia (jina lake halikuweza kupatikana) watoto kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi mfuko wa sukari.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi makopo ya maziwa. (Picha zaidi ingia hapa)

Sunday, May 30, 2010

Takwimu Zetu



Asante Da Subi
na TEDxDar (thx to
VijanaFM.com for the alert) kwa kuleta habari hizi.

Friday, July 25, 2008

Hata UKIWMI ni dili!

Habari ya kugeuza UKIMWI mradi, njia ya kujipatia mapesa tumesikia siku nyingi. Nani anaumia? Ni hao waathirika ambao misaada haiwafikii, huko waliopata mapesa wanajenga majumba ya fahari na kuendesha magari ya fahari.
Na mambo mengine. Hata haya hawana!

********************************************************************

Wanaougeuza ugonjwa wa ukimwi kuwa dili...

2008-07-25

Kutoka ippmedia.com

Na Haji Mbaruku, Jijini

Watanzania wametakiwa kutogeuza ugonjwa wa Ukimwi kama mradi wa kujinufaisha na badala yake kuwa na dhamira ya kweli katika kupambana na ugonjwa huo. Wito huo umetolewa na Dk. Thecla Kohi kutoka mtandao wa wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini, TNW + wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio Jijini Dar es Salaam.

Akasema hivi sasa zimeanzishwa taasisi nyingi za ukimwi ambazo baadhi yao ni kwa ajili ya maslahi binafsi. Dk. Kohi akasema hivi sasa kuna baadhi ya watu wanaonufaika kwa kujipatia mamilioni ya shilingi kwa kutumia kigezo cha kusaidia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo, akasema ukifuatilia mamilioni hayo, utabaini hayatumiki kwa shughuli iliyokusudiwa bali ni kwa ajili ya manufaa ya baadhi ya watu. Akasema Watanzania wengi bado wanahitaji kusaidiwa lakini wanashindwa kutokana na ugonjwa huo kugeuzwa kuwa mradi.

Akawashauri watu wasikae na kusubiri pesa ili kupambana na ugonjwa huo ambao bado unaendelea kupunguza nguvu kazi hapa duniani. Akasema sio vyema kila siku kukaa na kufikiria ni wapi zitapatikana pesa za Ukimwi wakati kuna mambo mengi ya kufanya.

kasisitiza kuwa, endapo taasisi za kupambana na ugonjwa huo zitafanya kazi zake ipasavyo, upo uwezekano wa ugonjwa huo kupungua nchini. Lakini endapo watu wataendeleza maslahi binafsi, hali ya Watanzania itaendelea kuwa mbaya kila kukicha.

Amesema ni lazima kuwa na dhamira ya dhati ya kupambana na ugonjwa huo badala ya kuendeleza maslahi binafsi.

SOURCE: Alasiri

Wednesday, May 07, 2008

Washington D.C. unaongoza kwa UKIMWI Marekani




Yaani hii habari inasikitisha. Habari zinasema kuwa Washington D.C., yaani mji mkuu wa Marekani unaongoza kwa kasi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa wa UKIMWI nchini. Tena wengi wao ni weusi! Jamani! Au ni kweli hiyo habari kuwa serikali ya Marekani ulifanya njama ya kumaliza watu weusi kwa ugonjwa huo! Wanasema kuwa unaenezwa kwa ngono na wanochoma sindano za madawa ya kulevya.


Zamani hapa Marekani walisema kuwa mashoga/wasenge ndo waliokuwa wanapata sana huo ugonjwa lakini sasa wanaanza kuona unaambukizwa kwa 'hetero' yaani mwanaume/mwanamke. Tumieni kondomu jamani! Kweli ni vitamu ukila peku lakini linda maisha yako!

************************************************************

A pioneering city in AIDS research, Washington, D.C., is ground zero for AIDS outbreaks. With infection rates in the nation’s capital now the highest in the country, health care workers have become foot soldiers in a battle to save Black women’s lives .


By Donna M. Owens

Torena White is pacing the sidewalk outside the Woodland Terrace housing project in southeast Washington, D.C., calling out to anyone who crosses her path. In her baggy jeans, sneakers and black leather jacket, White might be mistaken for one of the residents hustling drugs in this notoriously rough inner city neighborhood. But the 40-year-old is actually a health care worker, whose only street game is trying to stop the disease from spreading.

“Want to get tested? We’re doing HIV tests today,” she says, gesturing toward a makeshift clinic inside a nearby rec center, where her outreach team has set up tables with instant test kits. Her smile is warm, her voice friendly. “Come on in! We can hook you up with a test for free.”

One of countless foot soldiers on the front lines of what a local health official has dubbed a “modern, large and diverse epidemic,” she knows what is at stake. Simply put, D.C. now has the highest infection rate in the country.

A November 2007 health department report showed that one in every 40 D.C. residents is thought to be infected with either HIV or AIDS. Enter workers like White, among the team of doctors, social workers and outreach advocates at Family & Medical Counseling Service Inc., a community-based health care agency in the heart of D.C.’s Anacostia community.

“About 55 percent of our caseload is African-American women, most between the ages of 39 and 45,” says Angela Fulwood Wood, a social worker who is Family & Medical’s deputy director.

“Many of the women we see were diagnosed after a history of injection drug use or multiple sexual partners,” she says. “But increasingly we’re seeing women who have contracted this from heterosexual relationships with men.”

Inside the cramped offices that Family & Medical occupies on Martin Luther King Jr. Avenue, medical director Veronica Mapp-Jenkins, M.D., chats with one of her longtime patients. Carole, 48, was diagnosed with HIV 11 years ago.

“At first I was in denial. I didn’t want to deal with the sickness and pain,” says Carole, a pretty woman with smooth skin who once had a crack addiction. “But I have been coming here for ten years, and let me tell you, they are miracle workers.”

On any given day, some of the 75 Family & Medical workers can be found traveling the region in a Winnebago that serves as a mobile clinic, visiting jails, churches and festivals—anywhere they can reach people.Back at the housing project, several teenage boys, who should probably be in school but are hanging out instead, follow White inside and ask for condoms. One brags about needing “a whole box.” Another wants the “super” size.

White tells them if they agree to be tested, she’ll throw in a $5 gift card for groceries. One baby-faced young man, only 17, is game. Twenty minutes later, results from the instant test kit are back, and the teen learns his status: He is HIV-free.

The advocate notes how deeply personal this fight is. “This issue captured me,” White says. “If we can really reach people, if we can get them tested, maybe we can save them.”

Kutoka Essence.com

Saturday, December 01, 2007

Siku ya UKIMWI Duniani




Leo ni siku ya UKIMWI Duniani. Hakuna mTanzania asiyejua mtu aliaathirika au kufa kwa ugonjwa huo. Kama umetoka Tanzania siku nyingi halafu unarudi na unaanza kuuliza watu unaambiwa, "yule kafa, yule kafa zamani, yule tulimshasahau!" inasikitisha!

Afrika ugonjwa huo bado ni tishio. Juzi Tanzania walitangaza kuwa UKIMWI unaua kuliko malaria, maana watu 400 wanakufa kwa siku shauri ya huu ugonjwa. Zambia walisema idadi ya watoto waliopoteza wazazi wote wawili kwa UKIMWI unaongezeka. Afrika Kusini wanaume wanatembea na watoto wadogo wa hata miezi kusudi eti wapone ugonjwa huo!

Tatizo la Afrika ni kuwa inasambaza hasa kwa ngono. Waafrika wanapenda ngono. Utamsikia mtu anasema yuko tayari ku-risk kwa ajili ya raha ya muda mfupi. Na atasema "Oh, kila mtu atakufa!" Hiyo ni kweli lakini kwa nini ufupishe maisha yako kwa ajili ya raha?

Tumieni kondomu basi acheni kupenda kwenda Tigo, bila soxi! Utasikia msichana kakubali kufanya bila kondomu kwa vile mpenzi wake kamwambia, "Kama hutaki kavu ina maana hunipendi!"

Idadi ya watu wanaokufa na ugonjwa huo katika nchi ziliaoendelea zimepungua sana. Wagonjwa wapo. Nimeona wazungu waliothirika. Na hapa Marekani wengi ya waathirika ni weusi!

Tuombe Mungu kuwa Tiba ya kudumu ipatikane haraka. Dawa zipo za kurefusha maisha lakini hakuna dawa ya kuitibu kabisa ipotee mwilini mwa mtu.

Mungu atunusuru!

********************************************************************************
Kwa habari zaidi someni:

http://www.aids.org/

http://en.wikipedia.org/wiki/AIDS

http://aids.about.com/