Friday, July 25, 2008

Hata UKIWMI ni dili!

Habari ya kugeuza UKIMWI mradi, njia ya kujipatia mapesa tumesikia siku nyingi. Nani anaumia? Ni hao waathirika ambao misaada haiwafikii, huko waliopata mapesa wanajenga majumba ya fahari na kuendesha magari ya fahari.
Na mambo mengine. Hata haya hawana!

********************************************************************

Wanaougeuza ugonjwa wa ukimwi kuwa dili...

2008-07-25

Kutoka ippmedia.com

Na Haji Mbaruku, Jijini

Watanzania wametakiwa kutogeuza ugonjwa wa Ukimwi kama mradi wa kujinufaisha na badala yake kuwa na dhamira ya kweli katika kupambana na ugonjwa huo. Wito huo umetolewa na Dk. Thecla Kohi kutoka mtandao wa wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini, TNW + wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio Jijini Dar es Salaam.

Akasema hivi sasa zimeanzishwa taasisi nyingi za ukimwi ambazo baadhi yao ni kwa ajili ya maslahi binafsi. Dk. Kohi akasema hivi sasa kuna baadhi ya watu wanaonufaika kwa kujipatia mamilioni ya shilingi kwa kutumia kigezo cha kusaidia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo, akasema ukifuatilia mamilioni hayo, utabaini hayatumiki kwa shughuli iliyokusudiwa bali ni kwa ajili ya manufaa ya baadhi ya watu. Akasema Watanzania wengi bado wanahitaji kusaidiwa lakini wanashindwa kutokana na ugonjwa huo kugeuzwa kuwa mradi.

Akawashauri watu wasikae na kusubiri pesa ili kupambana na ugonjwa huo ambao bado unaendelea kupunguza nguvu kazi hapa duniani. Akasema sio vyema kila siku kukaa na kufikiria ni wapi zitapatikana pesa za Ukimwi wakati kuna mambo mengi ya kufanya.

kasisitiza kuwa, endapo taasisi za kupambana na ugonjwa huo zitafanya kazi zake ipasavyo, upo uwezekano wa ugonjwa huo kupungua nchini. Lakini endapo watu wataendeleza maslahi binafsi, hali ya Watanzania itaendelea kuwa mbaya kila kukicha.

Amesema ni lazima kuwa na dhamira ya dhati ya kupambana na ugonjwa huo badala ya kuendeleza maslahi binafsi.

SOURCE: Alasiri

No comments: