Showing posts with label Andrew Chenge. Show all posts
Showing posts with label Andrew Chenge. Show all posts

Tuesday, March 31, 2009

Mh. Andrew Chenge Kizimbani kwa Kuua!

Kutoka Michuzi Blog:

Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge (mwenye suti na tai) amepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili.

Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa mawili ni ya kusababisha vifo vya watu wawili, na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote.

Kesi hiyo inaunguruma mbele ya Hakimu Emerius Mchauru na imeahirishwa hadi April 30 mwaka huu. Aliachiwa kwa dhamana ya shilingi Milioni moja na mdhamini mmoja!
***************************************************
Wadau, ninafurahi kuona kuwa 'WAKUBWA' wanashtakiwa kama wananchi wengine siku hizi Bongo. Enzi 'zile' kesi kama hiyo inanyamazishwa kimya kimya! Nakumbuka kesi fulani miaka ya 80, mzito alimgonga mtu na gari kwenye barabara ya Port Access (wakati ule barabara nzuri kweli), na wala hakupelekwa mahakamani. Jamaa alikuwa anaendesha mwendo wa kasi. Hata kwenye gazeti habari haikuandikwa!