Showing posts with label Anguilla Festival 2010. Show all posts
Showing posts with label Anguilla Festival 2010. Show all posts

Thursday, August 05, 2010

Anguilla Festival 2010


Mshindi akijiandaa kuimba wimbo wake kuhusu umoja wa visiwa vya Caribbean.
Mshindi akiimba wimbo wake.
"YAH MAN! Anguilla kuzuri!"
Mashindano ya Calypson ya Vijana kwenye TV. Huyo binti hakuwa na sauti nzuri lakini nilipenda hiyo nguo aliyovaa ya kuwakilisha Anguilla.
Waziri Mkuu (Chief Minister) wa Anguilla Hubert Hughes

Wadau, jana jioni nilienda kwenye mashindano ya Calypso hapa Anguilla. Ilikuwa safi sana. Walishindana wanawake wanne na wnanauma 6. Mwanamke ndiye alishinda na nyimbo yake ya kuhusu visiwa vya Caribbean kuwa na umoja.

Nyimbo nyingi zilihusu siasa za Anguilla. Nimeshangaa maneno wazi wazi hakuna maficho. Mfano walisema kuna rushwa tele, waAnguilla wanaonewa na mabenki. Hawawezi kupata mikopo. Walilamika kuwa waChina wana haki kuliko waAnguilla na sasa wana maduka makubwa ya Hardware na restaurants tele.

Mwanamke fulani aliimba nyimbo kuhusu kupujunwa uroda na mume wake. Nimempenda jamaa 'Springer' ambaye ni jirani yetu hapa Blowing Point. Aliimba wimbo ambayo ilisema aliweza kutabiri kuwa kutakuwa na amani dunia nzima siku moja.

Lakini ajabu, jamaa fulani aliimba nyimbo kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni hapa kisiwani. Walitoa bango ya waziri mkuu na kuitumia katika wimbo! Nilishutuka, nikamwuliza mtu aliyekaa karibu na mimi ni nani huyo? Khaa! Jamani, kumbe nilikaa naye kwenye ferry kutoka Anguilla. Nilijua ni mtu wa maana jinsi watu walivyouwa wanamsalimia, lakini sikujua kamani waziri mkuu! Hakuwa na mbwembwe zile kama Bongo, mkubwa kubebewa begi, walinzi kibao, nk. Tena aliniomba kuazima kalamu kwa ajili ya kujaza fomu ya uhamiaji, lakini mtu mwingine alikuwa ameaimza. Yeye ndo alikuja kakaa na mimi na tulikuwa tunaongea, na nilitaka kumwuliza kama ana ndugu a shemeji yangu lakini sikumwuliza. Nadhani alijua mimi sikumtambua.

Habari zaidi baadaye.

Mnaweza kusoma habari za Anguilla Festival 2010 hapa:

http://www.axasummerfestival.com/results.php?eventID=24